"Wote tunafanyia kazi kuelewa tukio hili kubwa kwa kuwa ndio kwanza limetokea," aliongeza, akielezea kifo cha baba yake kuwa ni "pigo kwa watu wote duniani ambao walifurahia zawadi aliyokuwa nayo kama muigizaji.
Hafla ya heshima za mwisho kwa Connery itakayofanyika baadaye, kwa mujibu wa ofisa habari wake.
Lakini ilikuwa ni sinema maarufu ya 007, aliyoigiza akitumia Kiingereza chenye lafudhi ya Scotland akiigiza kama mpelelezi aliyekuwa na leseni ya kuua, iliyompatia umaarufu mkubwa duniani kote.
Alikuwa ni muigizaji wa kwanza kutoa maneno yasiyosahaulika ya "Bond, James Bond" na aliigiza filamu sita zilizotokana na mtunzi wa vitabu vya hadithi, Ian Fleming.
"Alikuwa na siku zote ataendelea kukumbukwa kama James Bond halisi," walisema watayarishaji filamu maarufu, Michael G. Wilson na Barbara Broccoli.
Mara kadhaa , mcheza sinema huyo kutoka Scotland alipigiwa kura na mashabiki ya kuwa muigizaji bora wa nafasi ya Bond, akiwashinda waigizaji wengine kama Daniel Craig wa sasa na Roger Moore.