Saturday, 29 February 2020

Mamlaka Ya Udhibiti Na Usimamizi Wa Bima Nchini[TIRA ] Yatoa Mafunzo Kwa Wanahabari Umuhimu Wa Bima Katika Jamii


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa bima nchini [TIRA]imetoa Mafunzoya kuwajengea uwezo Wanahabari umuhimu wa bima katika jamii  kwani ni moja ya suluhisho kwa Majanga  .


Akiwasilisha mada mbalimbali katika Mafunzo hayo jijini Dodoma,Mkurugenzi wa kuendeleza soko la bima na utafiti ,mamlaka ya Usimamizi wa bima Tanzania,Bi,Adelande  Muganyizi amesema bima husaidia kupunguza maumivu ya majanga mbalimbali ikiwa  ni pamoja na majanga ya moto,ajali,ukame,na mafuriko hivyo wanahabari wanatakiwa kuwa mabalozi wazuri  katika kuelimisha jamii umuhimu wa bima kwani huondoa umasikini.


“Majanga hayabigi hodi lakini bima inasaidia kupunguza sana maumivu yaliyotokana na majanga ,hivyo  tunatakiwa tuelewe sana haki ya usalama katika mali zetu pindi tunapokumbwa na majanga kwa hiyo tunapoongelea suala la bima ni usalama wa afya,Usalama wa mali zetu”amesema.


Aidha,Bi.Muganyizi ameanisha kanuni za msingi za  mkataba wa bima ni pamoja na kuwepo na uhusiano unaotambulika kisheria[Insurable interest],uaminifu wa hali ya juu[ultmost  faith], kumrejeshea mkata bima thamani halisi kabla ya janga kutokea pamoja na kuchangia hasara endapo mali moja imechangiwa na makampuni ya bima zaidi ya moja.


Akizungumzia kuhusu bima ya lazima,Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa bima[TIRA]kanda ya kati Stella Rutaguza amesema kwenye magari ya usafiri wa umma kila abiria aliyebebwa anatakiwa awe amekatiwa bima.


“Tukija kwenye suala hili naona kama kuna changamoto kidogo ,lakini kuhusu bima ya lazima inatakiwa kila abiria aliyebebwa kwenye gari la usafiri wa umma awe amekatiwa bima na mwenye jukumu hilo ni mmiliki wa gari husika,kama gari lako lina uwezo wa kibeba abiria 55 na sheria inataka hivyo hivyo ukate bima ya watu wa idadi kama hiyo”amesema .
Pia,Rutaguza amesema moja ya kanuni kubwa  ya bima ni kuwa hairuhusiwi kuikatia bima mali isiyokuwa ya kwako hata kama ni ya ndugu  huku akitaja aina mbalimbali za bima zikiwa ni pamoja na bima za kilimo,bima za ndoa,bima za dhima za umma ,bima za makosa ya kitaaluma ,bima za wizi ,bima za waajiriwa  ,bima za maisha,bima za elimu  na bima za vifo.


Meneja usimamizi wa Maendeleo ya Masoko ,Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa bima Tanzania[TIRA]Bw.Edgar Shao amesema TIRA ina jukumu la kusajili kampuni za bima pamoja na kutoa elimu kwa wananchi


Share:

CCM Shinyanga Kujenga Ofisi Za Chama Hicho Kwa Ngazi Zote

SALVATORY NTANDU
Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa shinyanga kimeziagiza kamati za siasa ngazi za vijiji,mitaa, kata na wilaya zote mkoani humo kuhakikisha wanajenga  ofisi za  matawi, vijiji, mitaa na kata ili kurahisisha upatikanaji wa  huduma kwa wanachama wake.

Agizo hilo limetolewa febuari 28 mwaka huu na Mwenyekiti wa (CCM) mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa katika maadhimisho ya miaka 43 ya (CCM) yaliyofanyika katika kijiji cha Bukindwasali katika halmashauri ya Ushetu wilayani kahama yaliyoenda sambamba na ukaguzi majengo ya chama hicho.

Mabala alisema kuwa kata ya Idahina imeongoza kimkoa katika ujenzi wa majengo ya chama ambapo mpaka sasa wamejenga ofisi za kata,kijiji na matawi 38 ya chama hicho ambayo yote yako katika hatua za kukamilika.

“Katika mkoa wa Shinyanga, kata ya Idahina mmeongoza kwa kujenga ofisi nzuri ya kisasa ya tawi la CCM Bukindwasali,niwaagize viongozi wangu CCM  wa ngazi za wilaya zote kuhakikisha wanawahamashisha wanachama wetu kujenga ofisi ili kurahisisha utendaji kazi”alisema Mabala.

Sambamba na hilo Mabala aliwataka wanachama wa CCM kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa ofisi za chama kwa ngazi zote ili kuwawezesha viongozi wapya waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa wanafanya kazi katika mazingira bora.

Kwa upande wake Naibu waziri wa ujenzi, na Mbunge wa jimbo la Ushetu,Elias Kwandikwa awamu ya Tano ya uongozi wa Dk John Pombe Magufuli imedhamiria kukijenga chama upya kwa kuhakikisha kila tawi,kijiji na kata vinakuwa na ofisi za kisasa za CCM.

“Niwaombe wanachama wenzangu jengeni ofisi za chama chetu mimi kama mbunge ninayetokana na CCM nitahakikisha nimalizia ujenzi wa majengo haya lengo letu ni kuwasaidia wanachama wetu kuhudumiwa kwa urahisi”alisema kwandikwa.

Naye Mwenyekiti wa CCM kata ya Idahina Masalu Walwa alisema kuwa katika eneo lake kumekuwa na mwamko mkubwa wa wanachama kushiriki katika ujenzi wa ofisi za CCM pamoja na majengo mengine ya Umma.

Aliongeza kuwa mbali na ofisi za CCM katika kata ya Idahina waliweza kujenga jengo la serikali ya kijiji,bweni la wasichana katika shule ya sekondari pamoja miradi mingine ya chama.

Mwisho.


Share:

Sales and Marketing at SINOTASHIP

Sales and Marketing Position  :   Sales and Marketing Location :   Dares Salaam Start  :   Immediately SINOTASHIP is a shipping based in Dar es Salaam. The company is looking for experienced SALES AND MARKETING personnel to join shipping department team. Responsibilities: Work out sales plans Develop potential clients and acquire bookings Manage customer relationship Achieve sales targets Submit sales… Read More »

The post Sales and Marketing at SINOTASHIP appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

DC Iringa: "Wanafunzi Wa Kike Msijirahisishe Tupunguze Ukatili"

Na Mwandishi Wetu Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela amewataka wanafunzi wa kike kutojirahisisha mpaka kupelekea kufanyiwa vitendo vya ukatili dhidi yao.

Ameyasema hayo leo mkoani Iringa wakati akiupokea Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia uliposimama mkoani hapo.

Ameongeza kuwa vitendo vya kikatili vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku hasa katika familia na vimekuwa vikifumbiwa macho na kumalizana kimya kimya.

"Msijirahisishe watoto wangu mnatupa tabu sana maana tumekuwa tunapambana na vitendo vya ukatili ninyi mnajirahisisha" alisema

Mhe. Kasesela amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la mimba na ndoa za utotoni na ulawiti kwa watoto wa kiume watoto wamekuwa wameharibiwa na kusbabishiwa maumivu na ukatili wa kisaikolojia.

Ameongeza kuwa Serikali imejipanga katika kuhakikisha inasimamia ustawi wa jamii ikiwemo kuwalinda na vitendo vya kikatili dhidi yao hasa kwa makundi maalum ya wanawake, Watoto na walemavu.

"Tusikae kimya tuseme tutoe taarifa kwa vyombo vya kisheria kuhusu vitendo vya kikatili vinavyotokea katika familia na jamii zetu"alisema.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi Imelda Kamugisha amesema vitemdonvyabukatili.vimekuwa vikitokea kwenye jamii zeru na kwa mujibu wa takwimu wanawake asilimia 30 walio kwenye ndoa wanafanyiwa ukatili wa kijinsia.

"Kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili Serikali imeongeza vituo vya huduma jumuishi na namba ya kutoa ripoti ya vitendo vya ukatili kwa watoto ili kuweza kuchukua hatua katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili" alisema.

Kwa upande wake Wakili kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na udhamini  RITA Janeth Mandawa ametoa wito kwa wanaume kuandika wosia ili kuondokana na vitendo vya kikatili vinavyowakumba wanawake wajane katika jamii zetu ili kuwezesha kuwapa haki zao stahili.

 "Sisi tunahusika na masuala ya wosia kuandika wosia sio kufa ila inasaidia kutoa maelekezo baada ya mume au mke kufariki ili tuondokane na vitendo vya ukatili"alisema.


Share:

LIUNDI AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA WANAWAKE WALIOFANIKIWA KATIKA UONGOZI


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi amewataka Waandishi wa habari nchini kuwapa nafasi kwenye vyombo vya habari wanawake waliofanya vizuri katika masuala ya uongozi ili kuwapa hamasa wanawake wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi.


Liundi ameyasema hayo, leo Jumamosi Februari 29,2020 wakati wa Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa

"Lengo la warsha hii kujenga na kuongeza uelewa na uwezo wa waandishi wa habari kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi. Hakikisheni mnawapa nafasi wanawake waliofanya vizuri katika uongozi ili kuhamasisha wanawake wengi zaidi wajitokeze kushiriki katika masuala ya uongozi na ngazi za maamuzi",alisema Liundi.

"Wale wanawake watakaojitokeza kugombea nafasi za uongozi wapeni nafasi kwenye vyombo vya habari,angalieni michango yao,itangazeni kwa jamii ili jamii iweze kuwaona. Kuna mifano bora ya wanawake ambao wamefanya vizuri sana katika masuala ya uongozi,wale mkiwa mnawapa nafasi ,basi jamii itaona wanawake wana uwezo mkubwa sana katika kufanya kazi",aliongeza Liundi.

Aliwataka waandishi wa habari kutumia mafunzo wanayopewa kujiimarisha katika kuripoti habari kwa mrengo wa kijinsia na kuhamasisha mila na desturi chanya.

"Tuongeze nguvu katika kuondoa mawazo mgando na mitazamo hasi,tuhakikishe tunapanda mawazo chanya wezeshi ili wanawake waweze kushiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi kwa wingi zaidi. Wanawake na wanaume wakishiriki katika ngazi za maamuzi kwa pamoja,kuna tija kwani inasaidia kuchochea maendeleo katika jamii",alisema.

"Wanawake ni zaidi ya asilimia 51 ya wananchi wa nchi za Afrika, kwa hiyo hatuwezi kuiacha hii asilimia 51 isishiriki katika kutoa maamuzi,ni muhimu sana kwa wanawake kushiriki katika michakato ya maendeleo,kushiriki katika nafasi za uongozi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo",alisisitiza Liundi.

Naye Afisa Habari wa TGNP Monica John alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kubadilisha mitazamo hasi dhidi ya wanawake katika jamii inayosababisha wanawake wasishiriki katika nafasi za uongozi.

John alisema kupitia warsha hiyo washiriki wataweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari hasa kusambaza ilani ya uchaguzi ya wanawake na kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawake na vijana katika uongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,Lilian Liundi akizungumza leo Jumamosi Februari 29,2020 wakati akifungua Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,Lilian Liundi akizungumza katika Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,Lilian Liundi akiwasisitiza waandishi wa habari kuwapa nafasi wanawake waliofanya vizuri katika masuala ya uongozi ili wanawake wengine waweze kuhamasisha kugombea nafasi za uongozi.

Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa. 
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa. 
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akielezea namna vyombo vya habari vinanatakiwa kushirikishwa katika kuhamasisha wanawake kushiriki katika masuala ya uongozi.
Mwandishi wa habari kutoka Redio Faraja mkoani Shinyanga, Anikazi Kumbemba akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari wa Star Tv mkoani Tabora, Mustapher Kapalata akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari kutoka Redio Faraja mkoani Shinyanga,Moshi Ndugulile akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa habari wa Redio Sachita mkoani Mara, Ahmad Macha akichangia mada wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Shinyanga wakifanya kazi ya Kikundi
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Mara wakifanya kazi ya Kikundi
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Tabora na Kigoma wakifanya kazi ya Kikundi.
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Simiyu na Njombe wakifanya kazi ya Kikundi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Kampuni ya Kuunda Mabasi ya Abiria Yaanzishwa Kibaha

Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya BM Motors iliyopo Kibaha mkoani Pwani, imeingia kwenye orodha ya kampuni zinazounda na kutengeneza mabasi ya abiria hapa nchini. 

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Jonas Nyagawa amesema, karakana hiyo iliyojengwa eneo la Zegereni katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani inatengeneza mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 45 hadi 57.  

Akiongea na Maafisa Habari kutoka Idara ya Habari – MAELEZO, amesema, kutoka na na msukumo wa mazingira wezeshi ya Serikali katika kuunga mkono Sera ya viwanda nchini, ameweza kufanikisha ndoto yake ya kuanzisha karakana hiyo miezi sita iliyopita. 

Amesema, ni fursa pekee katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inahamasisha Wananchi kuanzisha viwanda nchini ili kujenga uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa vijana.  

“Serikali imekuwa ikisisitiza uanzishaji wa viwanda ili nchi yetu ifikie uchumi wa kati na Wananchi waweze kuwa na kipato cha kati. Ili kufikia azma hiyo lazima kujengwe viwanda vingi na wananchi nao wapate ajira.” 

Bwana Nyagawa amesema, vifaa vinavyotumika kuunda mabasi hayo vinatoka sehemu mbalimbali, huku asilimia 55 vikitoka nje ya nchi. 

Tangu karakana hiyo ianze kufanya kazi tayari mabasi mawili yameshaundwa na yako katika hatua za mwisho za usajili ili kuanza kufanya kazi. 

“Kila kitu kinawezekana, Watanzania wanapaswa kuwa na uthubutu. Karakana hii inaunda mabasi na sio kwamba vifaa vyote vinatoka nje ya nchi, vingine vinapatikana hapa hapa nchini.” Amesema. 

Kufuatia uanzishwaji wa kampuni hiyo, hadi sasa imetoa ajira kwa Watanzania 15 huku baadhi yao wakiongeza ujuzi kutoka kwa Wataalamu wa nje ya nchi wanaofanya kazi na kampuni hiyo. 

Frank Ngewe ambaye ni fundi mkuu wa karakana hiyo amesema, ujenzi wa karakana hiyo umekuwa mkombozi mkubwa kwa vijana hususani wale waliopata mafunzo ya uchomeleaji vyuma, umeme, rangi n.k. 

“Kwanza tunamshukuru Rais wetu na Serikali kwa ujumla kwa kukazania Sera ya Tanzania ya Viwanda. Watanzania wengi hususan vijana hivi sasa wanapata ajira na kujikwamua kimaisha kutokana na kuanzishwa kwa viwanda nchini. ”Amefafanua zaidi Bw. Ngewe. 

Kwa upande wake Elibariki Maleshe ambaye ni fundi bodi wa mabasi katika karakana hiyo ameeleza kwamba, vijana wanapaswa kuchangamkia fursa za viwanda ili kupata uzoefu na kujifunza zaidi vitu vipya. 

''Vijana hasa wanaomaliza masomo ya ufundi wanapaswa kujikita kwenye masuala ya viwanda ili watakapomaliza masomo yao waweze kupata ajira kwenye viwanda vipya vinavyoanzishwa nchini.'' 

Wakati karakana hiyo ikiwa na miezi sita tu tangu ianze kufanya kazi ya kuunda mabasi, eneo hilo la Zegereni limetengewa zaidi ya ekari elfu moja kwa ajili ya viwanda vinavyojihusisha na shughuli  mbalimbali ikiwa ni kuiishi Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda.
 


Share:

Tumia Mwika Kujitibu Busha, Nguvu za Kiume

Mwika ni dawa  ya asili ya nguvu za kiume yenye kutibu matatizo kwa wakati mmoja ;

(1)Nguvu za kiume
(2) Kunenepesha Maumbile
(3)Kuchelewe kufika kileleni

Yajuwe matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

(1) Ngiri ya kupanda na kushuka
2.Korondani moja kuvimba
3.Tumbo kuunguruma kujaa gesi
4.Kisukari
5.Presha
6.Kiuno kuuma
7.Kutopata choo vizuri 

Pia tunatibu kisukari siku (14) vidonda vya tumbo siku (30), Miguu kufa ngazi, kuwaka moto .

Pia tunayo dawa ya mvuto wa mpenzi hata yupo mbali amekuacha atarudi na kutimiza ahadi zote mvuto wa biashara.

Wasiliana nasi kwa namba 0747100745 (Whatsap/ Kupiga kawaida)


Share:

Job vacancies at CRDB Bank Plc

Background CRDB Bank Plc is an African bank and a leading Financial Services Provider in Tanzania with current presence in Tanzania and Burundi, East Africa. The Bank was established in 1996 and was listed on The Dar Es Salaam Stock exchange (DSE) in June 2009. Over the years, CRDB Bank has grown to become the most innovative and… Read More »

The post Job vacancies at CRDB Bank Plc appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Supply Chain Officer – Procurement at Danish Refugee Council

Job title: Supply Chain Officer – Procurement Reporting to: Area Manager Location: Kyaka Overall purpose of the role: The main purpose of this position is to procure quality, value for money, goods and services for the field office in conformity with DRC/Donor Guidelines and policies and ensure the field office procurement plans are carried out. KEY DUTIES AND RESPONSIBILITIES… Read More »

The post Supply Chain Officer – Procurement at Danish Refugee Council appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WAZIRI UMMY MWALIMU: "TANZANIA HAINA MSHUKIWA WALA MGONJWA WA UGONJWA WA KIRUSI CHA CORONA (COVID - 19)"




Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu leo ametoa  taarifa ya mwenendo juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu inayosababishwa na virusi vipya jamii ya Corona (COVID - 19) ikiwa ni muendelezo wa taarifa tunazotoa mara kwa mara wakati wa milipuko. 


Katika Taarufa hiyo Waziri Ummy Mwalimu amesema Idadi ya wagonjwa duniani imeendelea kuongezeka ambapo hadi kufikia tarehe 27 Februari, 2020 jumla ya watu 83, 652 wamethibitika kuugua, na kati ya hao wagonjwa 2,858 wamefariki. Asilimia 94 ya wagonjwa waliothibitika duniani wapo nchini China. Hadi sasa jumla ya nchi 51 zimeripoti ugonjwa huu ambapo kati ya hizo tatu ni nchi za Afrika ambazo ni Algeria, Nigeria na Misri. 

Awmewatoa wasiwasi wananchi kuwa hadi sasa Tanzania haina mshukiwa wala mgonjwa wa ugonjwa wa kirusi cha corona (COVID - 19). Hata hivyo, bado nasisitiza kuwa tunahitaji kuendelea kuchukua Tahadhari kubwa ya kujikinga kupata ugonjwa huu kutokana na kuwa na muingiliano wa wasafiri kati ya Tanzania na mataifa mengine yaliyoathirika. 

Ameongeza katika taarifa hiyo kuwa Kutokana na hatari iliyopo ya maambukizi ya ugonjwa huu, Serikali imejiandaa kukabiliana na tishio la ugonjwa huu, hususan kupitia maandalizi ya muda mrefu ambayo tumekuwa tukiyafanya kukabiliana  na magonjwa hatari ya kuambukiza. Hatua mbalimbali tayari zimechukuliwa, na zinaendelea kuchukuliwa ambazo ni pamoja na:

Kuendelea na uchunguzi na ufuatiliaji wa wasafiri wote wanaoingia nchini kwenye mipaka yetu ikiwemo viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi kavu. 

Kwa kipindi cha kuanzia Januari 30 hadi 27 Februari mwaka huu, jumla ya wasafiri 11,048 wamechunguzwa katika mipaka yetu ambao wanatokea katika nchi zilizo na ugonjwa huu kwa sasa ikiwamo China. 

 Wizara inavyo vipima joto 140 (vya mkono 125 (hand-held thermo scanners) na vya kupima watu wengi kwa mpigo 15 (Walkthrough thermoscanners)) ambavyo vimefungwa na vinatumika katika maeneo yetu ya mipakani ikiwemo viwanja vya ndege na bandari.

Vilevile tumeongeza idadi ya wataalamu wa afya katika maeneo ya mipakani ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi 100 ili kuimarisha ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini kupitia maeneo ya mipakani.

Tumeandaa dawa, vifaa kinga na vitakasa mikono (Alcohol-based sanitizers) ambavyo tayari vipo kwenye Bohari za Dawa za Kanda kwa ajili ya kutumika endapo kutatokea mgonjwa.

Tumeandaa maeneo maalum katika mikoa yenye uwezekano mkubwa wa kupata wagonjwa kwa ajili ya kuwaweka washukiwa na kuwapatia matibabu wagonjwa.

Serikali imeimarisha uwezo wa kupima sampuli kupitia Maabara yetu ya Taifa ya Afya ya Jamii kwa watu wote wanaohisiwa kuwa na viashiria au dalili za ugonjwa huu ambapo ndani ya masaa 4 – 6 tunaweza kutoa majibu ya vipimo.

Tumeendelea kutoa elimu ya afya kwa umma kupitia njia mbalimbali ili wananchi na watoa huduma waendelee kuchukua tahadhari.

Pia, tumetoa mafunzo kwa watumishi wa sekta ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko na majanga ikiwemo jinsi ya kutoa matibabu ya magonjwa ya milipuko, kuchukua sampuli, uelimishaji na kuzingatia  kanuni za afya. 

Wizara imeisha waelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kubainisha vituo vya kutolea matibabu kwa washukiwa/wagonjwa wa covid-19 endapo watatokea ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba vituo hivi vina vifaa vyote muhimu vya kutolea huduma. 

Ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya majimaji yatokayo njia ya hewa wakati mtu mwenye ugonjwa huu anapokohoa au kupiga chafya, kugusa majimaji yanayotoka puani (kamasi), kugusa vitambaa au nguo zilizotumiwa na mtu aliyepata maambukizi ya ugonjwa huu au maeneo mengine yaliyoguswa na mtu mwenye virusi vya ugonjwa huu.

Hivyo ni muhimu kwa kila mwananchi kufanya yafuatayo ili kuzuia ugonjwa huu usiingie nchini:-

Kufuata kanuni za Afya kwa kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi au nguo uliyovaa sehemu za mikono (Kiwiko cha mkono kuzuia hewa/makohozi kusambaa na kuhatarisha wengine).

Kuzingatia usafi binafsi ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.

Kujizua kupeana mikono na kukumbatiana. 

Kuepuka kugusana na mgonjwa mwenye dalili za magonjwa ya njia ya hewa mwenye historia ya kusafiri maeneo au nchi zilizoathirika na ugonjwa huu.

Kuwahi kwenye kituo cha kutolea huduma za afya endapo utakuwa na dalili za ugonjwa huu.

Kutoa taarifa ya uwepo wa mtu mwenye dalili 
zinazohiswa kuwa za ugonjwa huu kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu nawe au piga simu namba 0800110124 au 0800110125 bila malipo.

Kusubiri au kuepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri, wasafiri wanapaswa wapate maelezo ya kitaalamu kabla ya kuondoka nchini. Kwa wale ambao wanafanya  biashara, tunashauri wafanye biashara mtandao katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa huu.

Aidha, Serikali inatoa maelekezo kwa Mikoa yote nchini kufanya yafuatayo:

Kuhakikisha ndani ya siku tatu wanawasilisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya jina la kituo ambacho kimetengwa maalum kwa ajili ya kuhudumia washukiwa au wagonjwa endapo watatokea katika kila Halmashauri.

Kuhakikisha Hospitali zote, za umma na binafsi, zilizoko katika maeneo yao zina eneo la muda la kumshikilia mshukiwa.

Kuimarisha uzingatiwaji wa Kanuni za kuzuia maambukizi (Infection Prevention and Control- IPC) kwa kuhakikisha watumishi wanahimizwa na wanapatiwa vifaa vinavyohitajika.

Aidha, Mikoa ihakikishe uwepo wa vitakasa mikono katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo mahoteli, nyumba za wageni, sehemu za ibada, shule, ofisi, sehemu za kazi na biashara

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kufanya mawasiliano kwa karibu na serikali ya China kuhusiana na watanzania 504 ikiwepo Wanafunzi waliopo mji wa Wuhan. Ninapenda kuwaondoa wasiwasi kuwa watanzania hawa wapo kwenye mikono salama. Hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kuhakikisha wako salama na mahitaji yao muhimu wanapatiwa. 

Akihitimisha taarifa hiyo ameendelea kusisitiza kuwa ushirikiano wa pamoja wa wananchi, sekta na wadau mbalimbali katika kuzuia na kukabiliana na mlipuko huu ni muhimu. Hii ni pamoja na wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kipindi hiki ambacho bado ugonjwa huu haujadhibitiwa na unaendelea kusambaa katika mataifa mengi. 

Amesema serikali inaendelea kufuatilia kwa umakini mkubwa hali ilivyo duniani na endapo itatengamaa tutawajulisha haraka. Nitoe rai kwa wananchi kutosambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika. 

Akimalizia kutoa taarifa hiyo amesema  Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya afya, likiwemo shirika la Afya Duniani (WHO) na sekta ya habari katika kuhakikisha kuwa afya za wananchi zinalindwa na elimu ya kutosha inatolewa.










Share:

WAKANDARASI WANAOSHINDWA KUTEKELEZA MIRADI YA REA KWA WAKATI KUKATWA FEDHA

KAIMU Mkurugenzi wa Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kushoto akizungumza wakati wa ziara  kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa wametembelea kwenye kazi walianzia Mkoani Manyara kijiji cha Terati na wapo mkoa wa Tanga katika wilaya ya Mkinga kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA Tanzania Julius Kalolo .

Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Madini na Nishati katikati akisisitiza jambo kwa  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kulia na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA Tanzania Julius Kalolo wakati wa ziara yao ya kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa kwenye mradi huo wilayani Mkinga
Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Madini na Nishati katikati akisisitiza jambo kwa  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kushoto na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA Tanzania Julius Kalolo wakati wa ziara yao ya kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa kwenye mradi huo wilayani Mkinga
Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Madini na Nishati  kushoto akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kushoto wakati wa ziara yao ya kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa kwenye mradi huo wilayani Mkinga kulia ni  Mwenyekiti wa Bodi ya REA Tanzania Julius Kalolo

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kulia akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo

KAIMU Mkurugenzi wa Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga amewaonya wakandarasi wanaozembea katika utekelezaji wa miradi hiyo nchini kwa kutokukamilisha ndani ya muda uliopangwa la sivyo watachukuliwa hatua za kimkataba ikiwemo kuvunjiwa mikataba na kukatwa fedha.

Mhandisi Maganga aliyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Mkinga alipotembelea vijiji vya Mbuyuni, Segoma, Sega na Mnyenzani ambapo pia walipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wakiwa wameambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Nishati na Madini Dustan Kitandula.

 
Ambapo alisema madhumuni ya ziara hiyo ni kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa wametembelea kwenye kazi walianzia Mkoani Manyara kijiji cha Terati leo wapo mkoa wa Tanga katika wilaya ya Mkinga.


Alisema kwamba madhumuni makubwa ya ziara yao ni kuona mradi wa Rea awamu ya tatu mzunguko wa kwanza ulianza mwaka Mwezi June 2018 na huo mradi ni wa
miaka miwili na sasa wamebakia miezi miwili au mitatu kumaliza mradi.


Alisema kwamba baada ya kutembelea mradi huo hawajaridhika sana na utendaji wake wa kazi wa mkandarasi wa Jarika na jinsi walivyoongea nae na aliwahaidi kufikia mwezi wanne atakuwa amemaliza hivyowananchi wa mkoa huo wawe na subira kati ya mwezi wa tatu au wa nne vijiji vyote ambavyo vinapaswa kupatiwa umeme vitakuwa vimenufaika.


“Labda niseme tu kwamba tutahakikisha wakandarasi wanaosimamia miradi huu wanakwenda kukamilisha ndani ya muda uliopangwa nawasipofanya hivyo taratibu za kimkataba zitachukuliwa kwanza watakatwa fedha tukiona
wanaendelea na mambo hayo hayo tutavunja mikataba “Alisema


“Pia niwaambie kwamba wakishindwa huo mradi wasitarajie watapata mradi mwengine watakuwa kwenye orodha ya wakandarasi ambao hawatapata kazi tena hivyo wakazane ili kuepukana na hali hiyo”Alisema Mhandisi Amon

 
Hata hivyo alisema aliwataka wakandarasi hayo kufanya kazi kwa bidii ili kampuni zao ziendelee kufanya kazi huku akieleza kwamba wao wanahitaji kufanya kazi na makapuni wazawa hivyo waonyeshe kwa vitendo uwajibikaji wao
katika kutekeleza miradi wanayokabidhiwa.


Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula alisema kwamba serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha inafanikisha zoezi la kupeleka umeme vijijini na kazi kubwa imefanyika
bahati nzuri yeye alishiriki kwenye jambo hilo tokea wanaanzisha Rea.


Alisema wakati Rea ikianzishwa walitenga fedha kutoka kwenye mafuta ya taa na mafuta mwengine ili ziende kutumika kutengeneza mradi huo ukiangalia
walipotokea na sasa serikali imefanyia kazi kubwa sana yapo mafanikio kutokana na kwamba kasi ya kupelekea umeme vijijini imekuwa kubwa sana.


Aidha alisema kwamba changamoto za REA awamu tatu ni katikati walipata tatizo la wakandarasi kupata vifaa nguzo ilikuwa ni tatizo huku uzalishaji kwenye viwanda vya nyaya napo kulikuwa na tatizo lakini sasa zimeondoka.


“Changamoto kubwa ni kwamba kwenye utekelezaji wa miradi bado kuna urukwaji wa maeneo unapelekea umeme kijiji x chenye vijiji vinne unakuta mkandasi ule wigo wa kufanyia kazi amepewa mdogo unakuta anapeleka kwenye vitongoji viwili vyengine vinabaki wamekuwa wakipigia kelele kila wakati”Alisema


Kitandula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Madini na Nishati alisema kwamba ni matumaini yake awamu ya tatu ya Rra mzunguko wa pili utaondoa hilo tatizo kwa wananchi.


Hata hivyo pia aligusia suala la ushirikishwaji viongozi kwenye maeneo husika ambapo aliwataka wakandarasi wapokwenda kwenye wilaya na vijiji wanavyotekeleza miradi huyo wahakikishe wanawashirikisha viongozi wa vijiji
na wilaya ili kuepka kuruka sehemu za huduma muhimu kama vile shuleni, nyumba za ibada na zahanati.


“Kwani wasiposhirikisha vuongozi hao matokea yake inasababisha sehemu za huduma muhimu kama vile Zahanati, nyumba za ibada na shule yanaacha kupatiwa umeme na hivyo kushindwa kunufaika na huduma hiyo muhimu”Alisema


Naye kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bwiti (CCM) Bakari Mkuya alishukuru kwa ujio wa Kaimu Mkurugenzi huyo kwenye wilaya hiyo huku akieleza kwamba changamoto zilizopo ni nyingi ambazo mbunge wao amejaribu kuzitatua.


Alisema kwamba kuna sehemu zina mapungufu miongoi mwa vijiji kuna maeneo mengine yamerukwa hasa vitongoji kwenye kata ambapo nguzo zimefika lakini kuna maeneo yameachwa hivyo wawasaidie kuwaambie wahakikishe wanayafikia


“Lakini tatizo kubwa ni kwamba kilio kikubwa baadhi ya nyumba vimerukwa tunamini hilo litafanyiwa kazi n mamlaka husika kuona namna kuondosha hali hii”Alisema Diwani huyo.
Share:

Lipumba: Hatutasusia Uchaguzi Tena....Tutaweka Wagombea Kote Tanzania Bara na Visiwani

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa pamoja na  Demokrasia Kuyumba  nchini lakini hawatasusia uchaguzi mkuu wa 2020, kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.

Prof Lipumba ameyasema hayo leo Februari 29, 2020, wakati wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa wa Morogoro, ambapo amefanya Mkutano wa ndani katika Jimbo la Morogoro Mjini.

"Tutahakikisha tunakuwa na wagombea katika maeneo yote ya Tanzania bara na visiwani, kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge, Udiwani na uwakilishi kwa upande wa Zanzibar', ameeleza.

Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 24, 2019, CUF pamoja na vyama vingine vya siasa vilisusia uchaguzi huo.


Share:

Mbogamboga Na Matunda Kupata Soko Katika Nchi Za Ulaya

Makampuni kumi na tano (15) yaliojumuisha wazalishaji pamoja na wasafirishaji wa bidhaa za Mbogamboga na Matunda wajiongezea fursa katika soko la Ulaya kufuatia Ushiriki wao katika Maonesho ya Kimataifa ya Mbogamboga na Matunda yajulikanayo kama Fruit Logistica 2020 yaliyofanyika tarehe 5 hadi 7 Februari, 2020  mjini Berlin nchini Ujerumani. 

Mazao yaliyovutia wanunuzi  na wadau wengine katika maonyesho hayo ni pamoja na parachichi, rasiberi, pasheni, ndimu zisizo na mbegu, njegere, snow peas na sugar snaps, maharage machanga (green beans), french Beans, babycarrots, aina mbalimbali za jamii ya pilipili, viungo vya chakula kama vile tangawizi, nana (mint), kitunguu jani (chives), tikiti maji na mafuta ya parachichi.  

Taarifa iliyotolewa nchini na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Balozi Dkt. Abdallah S. Possi imeeleza kuwa mafanikio ya ushiriki wa Tanzania yamekuwa mkubwa kutokana na makubaliano ya kimkakati yaliyofikiwa baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na wanunuzi wa mbogamboga na matunda wa nchi za Ulaya, hali inayoleta viashiria chanya vya kupata masoko makubwa. Makubaliano hayo yanatarajiwa kuimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi za Ulaya, na hivyo kuvutia uwekezaji katika sekta husika nchini. 

Wafanyabiashara wameweza kukutana na kuingia makubaliano na wanunuzi, wabia wa biashara na wadau muhimu kama vile Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) na Taasisi ya Kimataifa ya GLOBALG.A.P inayoshughulikia viwango vya ubora wa bidhaa za kilimo na mifugo.  Taasisi hizo ni wadau muhimu katika kuwawezesha wazalishaji kutumia njia salama, sahihi na endelevu katika uzalishaji na kuwaunganisha na masoko ya kikanda na kimataifa. Vilevile washiriki waliweza kujifunza teknolojia za kuzalisha, kusindika, kufungasha, kuhifadhi na kusafirisha mazao ya kilimo ili kukidhi mahitaji ya soko la Ulaya.

  “Binafsi nilikutana na mzalishaji kutoka Tanzania ambaye ameingia makubaliano na muwekezaji kutoka Ujerumani. Hii inamaanisha Maonesho haya pia yalikuwa ni fursa kwa wazalishaji wa Tanzania kutafuta wabia wa biashara” amesema Mhe. Balozi Possi.

Aliendelea kusema kuwa, mkakati wa Ubalozi ni kuandaa na kuratibu matukio maalum kama vile Maonesho, Semina, Mikutano ya ana kwa ana ya wafanyabiashara ili kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wadau muhimu wa nchi za Ulaya. Vilevile, Ubalozi wa Tanzania uliopo Barlin umekuwa ukihimiza ushiriki wa Tanzania katika Maonesho yanayofanyika nchini humo ili kutafuta fursa zaidi za kibiashara. 
 
Mhe. Balozi ameshauri wazalishaji kuimarisha umoja miongoni mwao ili wapate urahisi wa kuwa na wingi wa bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora vinavyohitajika katika soko kubwa la Ulaya kwa ujumla wake.

Fruit Logistica ni Maonesho makubwa ya matunda na mbogamboga katika Bara la Ulaya ambayo kwa mwaka huu yamevutia ushiriki wa waoneshaji zaidi ya 3,300 kutoka kila hatua ya mnyororo wa ugavi (supply chain) ambao walitoka katika nchi 93 duniani. Kadhalika, Maonesho yalivutia watembeleaji zaidi ya 78,000 kutoka nchi zaidi ya 135.

Kwa Tanzania, TanTrade kwa kushirikiana na Kituo cha Biashara ya Kimataifa (ITC) na Taasisi inayosimamia Wadau wa Matunda na Mbogamboga, Maua, Viungo vya chakula na Bidhaa zake (TAHA) iliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho hayo ikiwa ni matokeo ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa Market Access Upgrade Programme (MARKUP) wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa masoko ili kuongeza mauzo ya nje ya nchi kwa bidhaa za kilimo.


Share:

Kwacha Na Shilingi ya Tanzania Zarasimishwa Mpakani Tunduma Na Nakonde

Benki Kuu ya Tanzania na Benki Kuu ya Zambia zimerasimisha matumizi ya Kwacha ya Zambia na shilingi ya Tanzania kwenye mpaka wa Tunduma na Nakonde ambapo wananchi wataweza kutumia fedha za nchi hizo mbili katika shughuli zao za kila siku za kiuchumi bila kubadilisha.

Akizungumza kwenye hafla hio iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nakonde, Mhe. Field Simwinga pamoja na Viongozi wa Serikali na Wakuu wa Taasisi mbalimbali kutoka Zambia na Tanzania, Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando alieleza kuwa Urasimishaji wa Matumizi ya Kwacha na Shilingi utaongeza nguvu katika jitihada mbalimbali zilizokwishafanyika ili kuongeza chachu ya biashara katika eneo la mpaka wa Tunduma na Nakonde.

“Utaratibu huu utaondoa mlundikano wa Kwacha upande wa Tanzania. Kama mnavyojua, Wananchi wa Zambia wananunua bidhaa na huduma kwa wingi kutoka Tunduma kwa kutumia Kwacha wakati Watanzania hawawezi kununua vitu kutoka upande wa Zambia (Nakonde) kwa kutumia Shilingi. Kwa sababu hiyo kunakuwa na Kwacha nyingi upande wa Tanzania ambazo hatimaye zinaishia mikononi mwa wauzaji wasio rasmi”

Urasimishaji huo unategemewa  kuchochea shughuli za kiuchumi kwa kuwaondolea wananchi gharama za kubadili  fedha kwani kuanzia sasa watauza na kununua kwa kutumia Kwacha na Shilingi kwa pamoja.

“Ushiriki wa Benki zetu hapa Mpakani katika kununua na kuuza Kwacha na Shilingi kunawapatia wananchi huduma salama za ubadilishaji wa fedha, ambapo wataepusha  hatari ya Wananchi kupewa fedha bandia. Pia benki zitatoa viwango sahihi vya ubadilishanaji wa Kwacha na Shilingi hivyo kulinda thamani ya fedha zetu”, aliongeza.

Mhe. Irando alisema kuwa tukio hilo litaimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya Serikali ya Zambia na Tanzania na kuboresha hali ya maisha ya wananchi kwa kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Uzinduzi wa utaratibu huo ni utekelezaji wa Hati ya Makubaliano (MOU) iliyosainiwa tarehe 21 Septemba 2018, kama jitihada za serikali ya Zambia na Tanzania za kumaliza changamoto ya muda mrefu ya biashara holela ya fedha za kigeni katika mpaka wa Tunduma na Nakonde.


Share:

Tanzania Kushirikiana Na Ujerumani Kukabiliana Na Changamoto Zinazoikabili Sekta Ya Uhifadhi Wa Maliasilia Nchini

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Ujerumani katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya uhifadhi wa maliasili hapa nchini kwa lengo la kuiimarisha na kuiendeleza sekta hiyo.

Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya uhifadhi inayofadhiliwa na serikali ya Ujerumani katika Hifadhi ya Taifa Nyerere - Selous.

Akiwa ameambatana na Mwakilishi wa Kansela wa Ujerumani, Günter Nooke na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzani Regine Hess, Waziri Kigwangalla ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za uhifadhi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania.

Dkt. Kigwangalla amesema kuwa Ujerumani kupitia taasisi zake na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yakiwemo ya GIZ , KFW na Frankfurt Zoological Society (FZS) yamekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza shughuli za uhifadhi wa maliasili hapa nchini kwa kushirikiana na taasisi za uhifadhi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii akibainisha kwamba Sensa ya Tembo na Wanyamapori wengine wakubwa ya mwaka 2018 iliyofanyika katika Ikolojia ya Nyerere - Selous - Mikumi ni moja ya matokeo ya ushirikiano huo.

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi kubwa inazofanya za kuimarisha ulinzi wa maliasili na kudhibiti vitendo vya ujangili.

Amesema kuwa kuimarika kwa shughuli za uhifadhi nchini Tanzania ni matokeo ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi ya Tanzania na Ujerumani na kuongeza kuwa Ujerumani itaendelea kusaidia na kuunga mkono juhudi za uhifadhi nchini Tanzania kupitia programu na miradi mbalimbali.

Ziara hiyo pamoja na kujikita katika kuangalia miradi ya uhifadhi inayofanywa na Ujerumani katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere pia imeangazia maeneo mengine ambayo Tanzania na Ujerumani zinaweza kushirikiana kwa lengo la kuboresha hali ya uhifadhi pamoja na miundombinu katika hifadhi za Taifa.

Aidha, katika ziara hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Regine Hess na ujumbe wake walipata fursa ya kutembelea eneo lilipojengwa Kaburi la Askari wa Kingereza aliyeitwa Kepteni Selous ambaye alifariki dunia wakati wa Vita Kuu ya kwanza ya Dunia Januari 4, 1917 na jina la askari huyo kuwa chanzo cha jina la "Selous Game Reserve" - Pori la Akiba la Selous.


Share:

Wananchi Washauriwa Kutochakaza Noti Na Sarafu

Gavana  wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Profesa. Frolens Luoga amewashauri wananchi kutumia vyema fedha bila kuziharibu wala kuzichakaza kutokana na ubora na uthamani wa utengenezaji wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Prof. Luoga amesema, lazima fedha zitumike kwa uangalifu na kuwaasa wananchi kutumia fedha hizo bila kuzichakaza, kuzitupa wala kuziandika kwa kuwa fedha hizo zinapoharibiwa zinakuwa katika hatari ya kuharibiwa kabisa na mashine maalumu pindi zinapofika benki kuu, na kupelekea gharama ya kupata nyingine kupata fedha hiyo.

Profesa. Luoga amesema kuwa mabenki yana wajibu wa kusaidia benki kuu katika kutekeleza Sera ya Sarafu safi kwa kukusanya pesa zote zilizochafuka na zisizo na hali nzuri na kuzirudisha  benki kuu.

Amesema kuwa fedha ya nchi ina thamani kubwa hivyo lazima matumizi yake yawe ya uangalifu,

"Noti ya Tanzania inatengenezwa kwa gharama zaidi kwani inatengenezwa kwa pamba kwa asilimia 100 ukilinganisha na noti ya dola ambayo hutengenezwa kwa pamba kwa asilimia 75 ya pamba, na hiyo ni kutokana na matumizi" amesema.

Pia amesema kuwa Benki kuu itaendelea kushirikiana na vyombo vya dola katika kuwawajibisha wale wote watakaokutwa na hatia ya kuharibu pesa ambalo ni kosa la jinai.

"Kuchana noti ni kosa la jinai, wengi wamekuwa wakija benki kudanganya ili walipwe tumewabaini walioghushi na waliokamatwa wanachukulia sheria kwa kuwa hiyo sio biashara" Ameeleza Prof. Luoga.

Kuhusiana na malalamiko ya kupungua kwa pesa katika mzunguko Gavana huyo ameeleza kuwa;

" Kila asubuhi tunakutana na kuangaalia hali ya ukwasi katika mabenki na tunajua kila benki ina kiasi gani na tunaweza kutoa mkopo kwa mabenki ili waweze kufanya malipo" ameeleza

Amesema kuwa "Benki kuu inaangalia kiasi cha pesa katika  mabenki yote na kama benki haitakua na pesa tutaangalia ni kwanini na tutasaidia na ikitokea benki haina pesa kwa kutokidhi masharti kama benki tunachukua hatua nyingine" amesema Luoga.

Mwisho amewataka wananchi kutoghushi pesa ya nchi na kwa yeyote atakayekutwa na pesa bandia  atashtakiwa kwa  kosa la jinai na uhujumu uchumi.


Share:

DC Njombe Aagiza Kukamatwa Walimu Wafanyao Vitendo Vya Kikatili

Na Mwandishi Wetu Makambako
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameagiza kukamatwa kwa walimu mkoani Njombe watakaobainika kuwafanyia vitendo vya kikatiki wanafunzi ili kukomesha vitendo hivyo vinavyoendelea kutoka nchini.

Hayo yamebainika jana Makambako mkoani Njombe wakati msafara wa kijinsia kutokomeza ukatili ulipofika mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mhe. Ruth amesema kuwa Serikali haipingi adhabu ya viboko ila sio kutoa adhabu ya  viboko vya kupitiliza na kusababisha vilema na maumivu kwa wanafunzi.

Ameongeza kuwa suala la ukatili ni mapambano makubwa nchini hivyo jitihada zinahitajika kwa wananchi wadau na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha wanaunganisha nguvu pamoja kuondokana na vitendo vya ukatili.

Mhe. Ruth amevitaka vyombo vya usalama kuacha kufanya ukatili kwa kuchelewesha kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia na kusababisha ukatili wa kihisia kwa wahanga wa vitendo hivyo.

“Vyombo vya usalama mnachelewesha kesi mnaomba rushwa nawaomba vyombo vys usalama msiwe kikwazo cha kutopatikana kwa haki ya wahanga wa vitendo vya ukatili” alisema.

Akizungumza kuhusu msaada wa kisheria unaotolewa na Shirika la Legal Serivces Facility Joseph Magazi amesema kuwa wameweka nguvu katika kuisidia jamii katika matatizo ya kisheria kwa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria katika mikoa na wilaya kutoa elimu husika.

“Tumejipanga kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha tunaifikia jamii katika kutoa elimu itakayowezesha wenye matatizo mbalimbali ya kisheria kupata msaada na kuyatatua matatizo yao” alisema


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger