Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete ameitisha kikao
cha dharura cha Kamati Kuu (CC) kitakachofanyika Kesho mjini Dodoma,
huku ajenda kuu ikiwa ni kupitisha majina ya wagombea nafasi ya ujumbe
wa Halmashuri Kuu (NEC), zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali,
kuanzia ngazi za Wilaya mpaka taifa, na kwamba lazima zijazwe katika
kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kila mtu atimize wajibu
wake.
Kwa mujibu wa ratiba ya Chama hicho, Kamati ya Usalama na Maadili
itafanya kikao chake Julai 8 na kufuatiwa na Kamati Kuu Julai 9 ambayo
inatarajiwa kuchuja wagombea wote waliotangaza nia na kupata watano
ambao majina yao yatawasilishwa Halmashuri Kuu ya CCM (NEC) itakayofanyi
Julai 10 kuchuja wagombea hao na kubaki watatu watakaopigiwa kura na
mkutano mkuu kumpata mmoja. Mkutano huo mkuu utafanyika Julia 11 na 12.
Chanzo: MCL
0 comments:
Post a Comment