please pray for BANZA STONE
INASIKITISHA sana! Wakati hali
ya afya ya mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhani
Masanja ‘Banza Stone’ ikiwa ni mbaya nyumbani kwao Sinza jijini Dar es
Salaam, madaktari wanapata tabu na kusumbuka kuhusu ugonjwa wa fangasi
ya kichwa unaomsumbua.
Licha ya ugonjwa huo, pia kwa mujibu wa
ndugu wa
karibu, hivi sasa Banza pia anasumbuliwa na tatizo la maumivu
makali wakati wa kupata haja ndogo, kiasi kwamba hupiga kelele
anapofanya hivyo, huku akiwa pia haoni wala kusikia vizuri.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini
hivi karibuni, baadhi ya madaktari bingwa wa magonjwa ya kichwa wamesema
ugonjwa wa kichwa wa Banza, ambao kitaalamu huitwa Mucormycosis,
husababishwa na fangasi waitwao Murcorales ambao huingia ndani ya mwili
wa binadamu kwa njia ya hewa.
“Ingawa ugonjwa huu ni hatari, lakini
unatibika, ukivuta hewa yenye fangasi hao, huingia na kwenda moja kwa
moja kwenye mfumo wa damu kisha kuanza kuzunguka ndani ya mwili kufuata
damu. Baada ya kukaa kwa wiki kadhaa kwenye mfumo wa damu, huhamia
kwenye uti wa mgongo (spinal) ambapo huzaliana kwa wingi na kuanza
kusambaa kuelekea kwenye ubongo,” alisema dokta mmoja wa hospitali moja
kubwa jijini Dar.
Daktari mwingine wa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema ugonjwa unaomsumbua
Banza ni hatari kwani mashambulizi yake huwa ni makubwa na husambaa kwa
kasi kiasi kwamba wagonjwa wanaougua huwa na hali mbaya.
“Kati ya wagonjwa 100 wanaoumwa ugonjwa
huu, 30 hupoteza maisha,” alisema kwa kifupi daktari huyo akiuzungumzia
ugonjwa unaomsumbua nyota huyo ambaye yupo kitandani kwa zaidi ya miezi
mitatu sasa, akipatiwa matibabu katika hospitali ya Sinza-Palestina na
kurejea nyumbani kwao.
Jumatano iliyopita, wadau mbalimbali wa
muziki walimiminika nyumbani kwao baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa
mtunzi huyo hodari alikuwa amefariki dunia, ikiwa ni zaidi ya mara kumi
akizushiwa jambo hilo.
0 comments:
Post a Comment