wa 38 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho.
Chokala anaongeza idadi hiyo ambayo imejumuisha watu wenye majina na wasio na majina, wakiwemo mawaziri 10 na naibu mawaziri wawili. Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Chokala aliahidi kuimarisha matumizi ya bandari na reli nchini endapo atapewa ridhaa hiyo.
Chokala ambaye aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, alisema lazima afanye vitu vitakavyoongezea mapato ya Serikali. “Nchini kuna bandari ambazo zikifanya kazi vizuri zitaimarisha uchumi na kuongeza mapato kwa Serikali,” alisema.
Kwa upande wa reli alisema, endapo akiwa rais atahakikisha kunakuwa na treni nyingi za umeme ili kurahisisha sekta ya usafiri na kuinua uchumi.
Chokala, ambaye pia alikuwa mwandishi wa habari wa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, alisisitiza kupambana na masuala ya rushwa na ufisadi. Alifafanua kuwa rais anayepaswa kwenda Ikulu ni lazima awe msafi, anayetekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu na kanuni.
“Anayetakiwa kwenda Ikulu ni yule ambaye anatenda haki, anakemea rushwa na hana dhamira na tamaa ya kutaka kuiba”. Alisema kiongozi akiwa dhaifu na mla rushwa na watendaji wa chini yake watafuata nyayo za ufisadi.
0 comments:
Post a Comment