Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Omary na dereva wake pamoja na mtu mwingine mmoja, wamefariki dunia kufuatia ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, iliyotokea mchana wa leo katika mteremko wa Inyala Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni uzembe wa dereva wa gari la mkurugenzi aliyekaidi amri ya jeshi la polisi kusimama ili kupisha msafara wa malori.
Ajali hiyo imehusisha pia magari mengine mawili, likiwemo lori la kubebea mafuta, mali ya kampuni ya Lake Oil na lori lingiine la mizigo.
0 comments:
Post a Comment