Tuesday, 20 September 2022

WAKIMBIZI WA BURUNDI WATAKIWA KURUDI NCHI MWAO SASA

...
Msimamizi wa huduma za matibabu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye kambi ya wakimbizi Nduta wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma inayotolea na Shirika la Medical Team International Dk.Martin Mhina akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi Sudi Mwakibasi (wa pili kulia) kuhusu namna ya utoaji wa huduma hizo katika kambi hiyo. (Picha na Fadhili Abdallah)
Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo nchini Tanzanaia Dk.George Mwita (kushoto) akimtembeza Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi Sudi Mwakibasi (kulia) katika kituo cha utoaji wa huduma za matibabu za magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kwenye kambi ya wakimbizi ya Nduta wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kinachoendeshwa na Shirika hilo wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi Sudi Mwakibasi (kulia) akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha utoaji wa huduma za matibabu za magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kwenye kambi ya wakimbizi ya Nduta wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kinachoendeshwa na Shirika la Medical Team International (kushoto) Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo nchini Tanznaia Dk.George Mwita.
Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi Sudi Mwakibasi (kulia) akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha utoaji wa huduma za matibabu za magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kwenye kambi ya wakimbizi ya Nduta wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kinachoendeshwa na Shirika la Medical Team International (kushoto) Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo nchini Tanznaia Dk.George Mwita.
Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya Nchi Sudi Mwakibasi akizungumza kwenye kambi ya wakimbizi ya Nduta wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma na kuwataka wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa kwenye kambi hiyo kurejea nchini kwao kwa hiari




Na Fadhili Abdallah,Kigoma


WAKIMBIZI wa Burundi wanaohifadhiwa kwenye kambi ya Nduta wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wametakiwa kuwekeza nguvu na akili zao katika kufikiri kurudi nchini kwao badala ya kutumia muda mwingi kuomba kuimarishwa kwa huduma kwenye kambi hiyo ya wakimbizi.


Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Sudi Mwakibasi alisema hayo akizungumza na wakimbizi wa Burundi kwenye kambi hiyo wakati wa uzinduzi wa kituo cha kutoa huduma za afya ya msingi na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kinachoendeshwa na Shirika la Medical team International.


Mwakibasi alisema kuwa kwa sasa nchi ya Burundi ina amani na watu wengi wamekuwa wakifanya kazi zao za maendeleo hivyo haiingii akilini kuona kuwa bado wapo watu wengi wa nchi wanahifadhiwa kwenye makambi nchini Tanzania kama wakimbizi.


“Serikali za Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa tumekubaliana wakimbizi warudi kwao kwa hiari baada ya kujiridhisha uwepo wa amani ya kutosha lakini bado idadi ya wakimbizi wanaojiandikisha kurudi ni ndogo sana na hali hii itachukua muda mrefu wakimbizi kurudi kwao hivyo kwa hali hii tunawataka wakimbizi wajiorodheshe kwa wingi kurudi nchini kwao,”Alisema Mwakibasi.


Mkurugenzi huyo alisema kuwa pamoja na kuboreshwa kwa baadhi ya huduma kutokana na hali ya kibinadamu lakini mashirika mengi hayataendelea kutoa huduma kambini humo kwani kwa sasa wakimbizi hao hawana hadhi ya kuwa wakimbizi kutokana n a nchi yao kuwa na amani na iko tayari kuwapokea warudi.


Awali akizungumza kabla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Medical Team International (MTI),Dk.George Mwita alisema kuwa uzinduzi wa kituo hicho cha matibabu unaangazia magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ambayo yamekuwa na uhitaji wa kupata huduma maalum.


Dk.George alisema kuwa zipo huduma za kawaida za matibabu zinazotolewa kambini hapo lakini kuhitajika kwa huduma za matibabu za magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiwa ikiwemo Presha,kisukari, magonjwa ya mfumo wa hewa, kifua kikuu,HIV na sikoseli.


Alisema kuwa pamoja na uwepo wa madaktari maalum wa magonjwa hayo pia kituo hicho kitakuwa na huduma za upimaji na utoaji wa dawa kwa magonjwa hayo kukiwa na vifaa muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya upimaji na utoaji huduma za matibabu za magonjwa yasiyo ya kuambukiza.


Baadhi ya wakimbizi wakiongea baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho walisema kuwa imekuwa faraja kubwa kwao kwani katika hospitali za kawaida zilizopo ndani ya kambi hiyo ya wakimbizi magonjwa hayo yalikuwa yakichanganywa na kutibiwa kama magonjwa mengine.


Mmoja wa wakimbizi hao, Ndaisaba Gelard alisema kuwa wamefarijika kufuatia kufunguliwa kwa hospitali hiyo kwani kwa sasa wanapata huduma za upimaji na kupewa dawa kulingana na magonjwa yako tofauti na hospitali nyingine walizokuwa wakipata tiba ambazo wakati mwingine baadhi ya vipimo havikuwepo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger