Thursday, 15 September 2022

PESACO YAWATAKA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YASIYOSAHIHI YA KIMTANDAO

...

************************

SHIRIKA la PESACO katika utekelezaji wa mradi uitwao "the Impact of Cyberbullying on Adolescents" unaofadhiliwa na Womenfund leo Septemba 14,2022 wametembelea katika shule ya Sekondari Mugabe kutoa elimu ya masuala ya unyanyasaji wa kimtandao.

Akizungumza katika utekelezaji wa mradi huo, Afisa Mradi wa Cyberbullying on Adolescents chini ya Shirika la PESACO, Bi.Eva Mwambongo amesema wamewaeleza wanafunzi ni namna gani wanaweza kujiepusha na suala zima la unyanyaaji wa kimtandao.

Amesema unyanyasaji wa kimtandao unaweza ukasababisha kushuka kwa kiwango chao cha elimu shuleni pamoja na kuwafanya kuwa na matatizo ya kiakili na kihisia.

"Wanafunzi wanatakiwa kutunza taarifa zao binafsi na wasiweze kuwaamini watu ambao ni wageni na kutuma na kusambaza picha zao hovyo kunaweza kupelekea akakumbwa na unyanyasajiwa kimtandao". Amesema

Katika utekelezaji wa mradi huo katika shule ya Sekondari Mugabe walikuwa na wadau mbalimbali ambao wamewawezesha kufanikisha jambo hilo akiwemo Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Ubungo pamoja na mwakilishi kutoka jeshi la polisi.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger