Wanamitandao wamechekeshwa na video iliyozagaa mitandaoni iliyomwonesha mvulana mdogo, akimtaka mhubiri kumuombea mama yake aliyemuiba mume wa mtu.
Video hiyo iliyovuma, inamwonyesha mama wa mvulana huyo akijifunika uso wake kwa aibu, huku mwanawe akifichua siri ya aibu
Mvulana mwenye umri wa miaka tisa, aliamua kutoboa siri mbele ya umati wakati wa ibada ya kanisa, na kuwashangaza wengi aliposema kwamba mamaake mzazi anaishi na mume wa mtu hivyo kumtaka pasta amkemee ili aondoke
Mpango wa kando Mvulana huyo mwenye ujasiri alichukua kipaza sauti bila ya kuogopa, na kumuita pasta amuombee mpenzi wa mama yake ili ahame nyumbani kwao, wanakoishi naye.
Video ya hiyo ya kusisimua ilipakiwa kwenye Facebook na Alberto Nyakundi Amenya BananaPeddler aliyesema kuwa:
"9-year old. Kwa mara ya kwanza pastor amechanganyikiwa. Sasa haka kakijana ni ka-genius ama ka-saitaan?" Tazama video ifuatayo ya jinsi mtoto huyo wa kiume alivyomuaibisha mama yake.
Video hiyo iliibua hisia mseto mitadaoni na zifuatazo ni baadhi ya maoni yaliyotolewa:
Francis Kiarie aliandika: "Haya mambo hutokea. Mambo ambayo hufanyika gizani, hujitokeza hadharani kwa nguvu ghafla bin vuu. Inawezekana."
Moses Nyabuto aliandika: "Jiepusheni na haya makanisa ya mitaa. Ni heri ubaki nyumbani kwako ujiomboe na kusali ikiwa inawezekana."
Oindo Douglas Mokaya aliandika: "Na wanasema wako 'I'm single but comfortable'. Yesu ndiye Bwana yangu kumbe ni Baba Jemo mume ya Njeri."
0 comments:
Post a Comment