Rapper
Afande Sele amesema wasanii hawajanufaika na ubunge wa Joseph Mbilinyi
aka Sugu licha ya kumsaidia kumpigia kampeni katika uchaguzi uliopita.
Akizungumza
na Planet Bongo ya East Afrika Radio, Afande alisema Sugu ameshindwa
kuwatumikia wasanii na kujinufaisha yeye mwenyewe.
Sisi
tuliamini akienda kule ndio mdomo wetu, kasahau kabisa wasanii wenzake,
alisema. Kipindi ambacho wasanii wa antivirus wanalalamika kwamba
kawatosa porini, akasema yeye sio mbunge wa wasanii ni mbunge wa Mbeya.
Huyu ni msaliti kwa wenzake, sasa mtu msaliti namna hii jinsi kumuondoa
ni sisi kuamua kuingia bungeni wenyewe kupigania maslahi yetu,
aliongeza.
Baada
ya kauli hiyo, Sugu amemjibu kwa kusema kuwa yeye hakuwa mbunge wa
wasanii bali alikuwa mbunge kwa ajili ya watu wake wa Mbeya mjini.
Nafikiri
hafuatilii bunge, unajua uzuri wa vitu vya bunge vinaenda kwa rekodi,
labda atakuwa hafuatili bunge. Lakini kwa wanaofuatilia bunge wanajua.
Mimi sio mbunge wa wasanii, mimi ni mbunge wa Mbeya mjini, alisema Sugu.
Kwahiyo
chochote ninachokifanya bungeni ninakifanya kwa mapenzi yangu na pia
kama waziri kivuli. Kwa msanii anayefanya kazi sawa ila kwa mtu
anayelala lala kama yeye lazima atakufa njaa. Lazima utakufa njaa lakini
kwa msanii kama Professor Jay, msanii kama Shetta wana- appreciate kazi
ambayo tunaifanya bungeni kwa kauli zao.
0 comments:
Post a Comment