Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni kuelekea nchini Italia kwa ziara
ya siku nne ya kiserikali.
Katika
ziara hiyo Maalim Seif anamuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Moh’d Gharib Bilal kwenye maonyesho ya
biashara ya kimataifa yanayofanyika mjini Milan nchini Italia.
Maonyesho
hayo ya kimataifa yanazishirikisha zaidi ya nchi mia moja na arobaini
(nchi 140), na yanatarajiwa kuhudhuriwa na wageni wapatao milioni 20
kutoka pembe zote za dunia.
Pamoja
na mambo mengine, maonyesho hayo ambayo pia yanazishirikisha taasisi za
kimataifa, yanabeba ujumbe wa umuhimu wa chakula chenye siha kwa afya
bora za wananchi duniani kote, pamoja na kuzingatia matatizo ya
upatikanaji wa chakula hicho duniani.
Kwenye
ziara hiyo Maalim Seif anaambatana na viongozi mbali mbali wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na watendaji wengine wakiwemo Waziri wa
Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Waziri wa
Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi Mhe. Haji Mwadini Makame, Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Zahra Ali Hamad na Mwakilishi wa Jimbo
la Ole Mhe. Hamad Massoud Hamad.
0 comments:
Post a Comment