ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
Martha kule nyumbani, akakumbuka kwamba alipanga kwenda kufanya usafi nyumbani kwa Roi, hivyo alijiandaa, akatoka akipanga kwamba atakapokaribia kufika ampigie simu Roi kumwambia ampitishie funguo za nyumba.
JIACHIE MWENYEWE SASA…
Aliwaaga wapangaji wenzake akisema anatoka mara moja…
“Jamani natoka, nitarudi lakini,” alisema Martha akiwa tayari kwenye ngazi.
“Poapoa.”
Martha alichukua usafiri wa Bajaj, akapanda hadi alipokuwa akikaribia nyumbani kwa Roi, akampigia simu…
“Uko wapi baby?”
“Niko Magomeni.”
“Mi nakaribia kwako, nipitishie funguo nifanye usafi.”
Roi moyo ulimlipuka puu! Maana alijua Martha atakumbana na mama Anna, kama si nje basi mitaa hiyo.
“Mh!” aligunia moyoni, akatafuta uongo wake…
“Funguo niliziacha nyumbani kwako mbona.”
“He! Kweli?”
“Yes! Kwenye nini?”
“Kwenye begi langu, kama siyo basi kwenye suruali niliyovaa jana. Kacheki.”
Martha alimwamuru dereva wa Bajaj ageuze amrudishe nyumbani kwake. Wakati anageuza, mama Anna alimwona mita chache, yeye alikaa kwenye kiduka jirani na kwa Roi, akauchuna, akazungusha sura.
Alipoiona Bajaj imepotea, akampigia simu mpangaji mmoja…
“Martha yuko hapo?”
“Ametoka.”
“Alisema anakwenda wapi?”
“Hajasema, kasema natoka kidogo tu. Vipi kwani?”
“Mh! Kaja mpaka nje kwa huyu jamaa yake, kageuza. Yuko na Bajaj.”
Wakati mama Anna akiendelea kuongea na mpangaji mwenzake huyo, mara simu yake ikawa inaita, kuangalia ni Roi, akakata simu hiyo na kupokea ya Roi…
“Niambie baba.”
“Uko wapi mama?”
“Niko nje kwako hapa.”
“Ha! Martha hajakuona kweli? Maana kaja hapo.”
“Nimemuona, lakini yeye hajaniona. Kwani kaja kufanya nini tena?”
“Eti alikuja kufanya usafi. Nimemdanganya kwamba funguo ipo nyumbani kwake.”
“Kwa hiyo kaifuata?”
“Kaifuata. Sasa mimi nakuja hapo dakika tano tu.”
“Poa.”
Baada ya dakika tano kweli, Roi akawa amefika nyumbani kwake, akashuka, akafungua geti na kuingiza gari ndani. Akamwingiza na mama Anna ndani, tena mpaka chumbani.
“Uzuri wake hata akija, hawezi kuliona gari ndani. Nitamwambia niko njiani bado,” alisema Roi kwa sauti ya kuibiaibia.
Martha alifika na kuangalia funguo sehemu zote alizoambiwa, hakuziona, akampigia simu…
“Baby, sijaona funguo bwana, utakuwa nazo kwenye gari, hebu angalia vizuri.”
“Ngoja niangalie.”
“Kwani uko wapi?”
“Nipo barabarani bado.”
“Poa.”
Roi alifunga milango yote, akazama chumbani ambako alimkuta mama Anna akiwa amejilaza na ameshajichojoa nguo zote. Alikuwa kama alivyozaliwa. Na kwa kujua hilo, alipomwona Roi ameingia, akajitingisha makusudi pale kitandani, Roi hoi. Alianza kuhema kimahaba.
“Si unaoga kwanza baba?” aliuliza mama Anna akiitoa sauti kwa kupitia kwenye tundu za pua.
“Yes,” Roi alisema kwa sauti nzito huku macho yako kwenye mwili wa mama Anna pale kitandani.
Roi alizivua nguo zake na kuzitupa chini kama vile hatazivaa tena katika maisha yake…
“Teh! Teh! Teh!” alichekacheka kwa kicheko cha uchu huku akimfuata mwanamke huyo pale kitandani…
“Jamani baba, si umesema unakwenda kuoga kwanza.”
“Yeah! Lakini kuna nini kama nita…nita naniihii kabla sijakwenda kuoga..? Teh! Teh!” Roi alibabaika. Hapo tayari alikuwa mwilini mwa mama Anna. Alilala na kumpapasapapasa sehemu mbalimbali za mwili.
Mama Anna naye akachangamka maana aliguswa, akapatwa na hisia za mapenzi, hasa kwa joto la Roi…
“Kwa hiyo utaoga baadaye?” aliuliza mama Anna…
“Au ngoja nikaoge sasa hivi,” alisema Roi, mama Anna akamzuia maana sasa na yeye mzuka si ulishapanda!
“Hakuna hapa, kama ungetaka ungekwenda tangu muda ule. Mimi mwenzio tayari sasa,” alisema mama Anna.
“Tayari nini?” aliuliza Roi akijifanya hajui lakini ukweli ni kwamba alikuwa anajua tayari nini.
“Kwani hujui?”
“Sijui,” alijibu Roi.
Mama Anna akapeleka mkono wake mmoja na kushika maiki akiashiria utayari wake uko wapi.
Roi naye akaunganisha hisia, wakabilingishana mpaka wote wakawa hoi, wanahema tu. Mama Anna akavuta mpira uwanjani, mchezo ukaanza kupigwa huku ushangiliaji ukiwa mkubwa kwa pande zote mbili.
Maneno yote, mama Anna aliyatumia, Roi akawa kama amepungukiwa akili, alisema yasiyosemwa.
***
Martha alipoona muda unakwenda aliamua kutoka tena akiamini, Roi alishaziona funguo na sasa atapitia nyumbani kwake ili wakutane.
Alipanda Bajaj tena mbele ya wale wapangaji wenzake.
Ile anapotea tu, yule mpangaji aliyepigiwa simu na mama Anna akamtumia meseji mama Anna…
“Martha katoka hapa tena, nahisi anakuja hukohuko.”
Mama Anna hakupata nafasi ya kuisoma meseji hiyo kwani wakati inaingia ndiyo kwanza yeye alikuwa katikati ya mashambulizi uwanjani akitafuta ushindi na alishatangaza kwamba anakaribia kuupata.
Hata alipoupata, Roi hakumwachia ili na yeye apate pointi yake moja ili kusiwe na wa kumzidi nguvu mwenzake. Mama Anna alitumia ufundi kidogo tu, Roi akawa akihangaika mpaka jasho jembamba likamchuruzika, ambapo mama Anna alilimudu kuliondosha kwa taulo.
***
Martha alifika nje ya nyumba na kumpigia simu Roi. Simu iliita kule chumbani, Roi kwa vile alishashinda, akatoka kwa mama Anna na kuiwahi…
“Du! Wajina wako anapiga,” alisema.
“Sasa. Anaweza kuwa nje?” aliuliza mama Anna…
“Inawezekana,” alisema Roi lakini hakuipokea simu hiyo.
Mama Anna naye akakumbuka, simu yake akaifuata, akakutana na ile meseji. Alipoisoma, akamwonesha Roi…
“Martha katoka hapa tena, nahisi anakuja hukohuko.”
Roi alitumbua macho pima, akasimama akiwaza, akasema…
“Kwa hiyo yupo nje hapo?”
“Ndiyo maana yake,” alijibu mama Anna.
Martha alishangaa simu ya Roi kuita bila kupokelewa kwani si kawaida yake.
Akaenda kwenye kile kiduka cha jirani…
“Dogo hujambo?” alimsalimia muuzaji.
“Sijambo.”
“Eti, huyu kaka anayekaa hapa huwa anafika muda gani?
0 comments:
Post a Comment