MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya
Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye aliwahi kuathirika na utumiaji
wa ‘unga’, hivi karibuni alitinga ofisi ya kitengo cha kupambana na
kudhibiti madawa ya kulevya na kuomba kupatiwa majina, idadi na sehemu
walipo watumiaji wa mihadarati hiyo ili aweze kuwasaidia kwa kuwapa
somo, kitu kinachotafsiriwa kama bado unamtesa.
Ray
C katika harakati zake akifanya mahojiano na msanii wa Hip hop, ambaye
yupo mbioni kuachana na madawa ya kulevya, Ibra the Hustler.
Ray C anadaiwa kufika katika ofisi hizo,
Aprili Mosi, mwaka huu, saa nne asubuhi hali iliyozua gumzo kwa askari
waliomuona ambao walijiuliza kitu alichokifuata.
Akizungumza na Uwazi, kamanda wa kitengo
hicho cha madawa ya kulevya, Godfrey Nzowa alikiri kufika kwa msanii
huyo ofisini kwake na kutoa madai hayo lakini alimwelekeza kwenda
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani huko kuna kitengo kinachoshughulika
na watu wenye matatizo ya akili wakiwemo watumiaji wa madawa ya kulevya.
Kamanda huyo alionesha kufurahishwa na
kitendo cha msanii huyo ambaye pia anamiliki taasisi yake yenye lengo la
kuwasaidia waathirika wa matumizi ya madawa hayo kwa kuwapa elimu,
akisema atatoa msaada mkubwa kwa wenzake.
Aliwataka watumiaji wa madawa hayo ambao
wameshindwa kuacha, wamfuate msanii huyo ili awape elimu na amewaonya
wote wanaotumia na kusafirisha madawa hayo.
“Wote wanaotumia na kuuza madawa hayo
waache mara moja kwani kikosi kazi kinachopambana na biashara hiyo
kimejipanga kila kona ili kukomesha biashara hiyo haramu,” alisema
Kamanda Nzowa
0 comments:
Post a Comment