Taxi
ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku
askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu
katika eneo la tukio..
BASI
aina ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa
eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali
iliyojeruhi zaidi ya watu 30. ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika
ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la
abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali
ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya jana. Tukio hilo
limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama
"Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao
wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali
hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus hilo la abiria,lenye
namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper
Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace.
Akizungumzia
hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa
mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na
waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa
majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27
wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha
makubwa.
0 comments:
Post a Comment