Nick
Van Lawick (13 , ambaye ni chotara anayetokana na mzazi wa Kijerumani
na Kitanzania, anasema akikua na kuwa mchezaji mkubwa kama anavyoota.
Siku zote
katika maisha ni muhimu kuwa na utamaduni wa kuheshimu ndoto zetu hata
kama tunadhani ni ndoto ndogo. Kuziheshimu ndoto zetu na kuzitimiza,
kunahitaji nidhamu ya ziada, ingawa wapo wanaozifikia andoto zao kwa
bahati.
Wengi
husema wanataka kutimiza ndoto zao, lakini ni wachache hufanikiwa
kutimiza ndoto zao. Hata hivyo kwa kuwa binadamu tuna ndoto tofauti
tofauti ni ngumu kuwa na kanuni moja ya jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Mtoto
Nick Van Lawick (13), anayesoma shule ya kimataifa ya Dar es Salaam
Independence School, ana ndoto ya kuichezea klabu ya Barcelona ya
Hispania na anatarajia atatimiza ndoto hiyo.
Hiyo
inatokana na kipaji alichonacho cha soka na mipango iliyofanywa na
wazazi wake, ambao watamkutanisha Nick na mtaalamu wa viungo wa klabu ya
Barcelona, Juanjo Brau.
Baba mzazi wa Nick anayeitwa Hugo van Lawick anasema: “Nick amepata nafasi ya kwenda kupewa mafunzo na Brau.
“Mama
yangu Jane Goodall ni rafiki wa karibu wa Brau na mama yangu anafahamu
kipaji cha mpira cha mjukuu wake, ndio maana aliona awasiliane na rafiki
yake kuangalia nafasi ambayo Nick anaweza kujiendeleza zaidi kisoka.
“Brau
alishauri kuwa Nick aanze kwa kumpa mafunzo ndipo mchakato wa kumtafutia
nafasi katika timu ya vijana ya Barcelona ufanyike.”
Kwa
upande wake Nick, anayesoma kidato cha pili, anasema anapenda sana mpira
na muda wake mwingi huutumia katika mambo yahusuyo mpira huku akiipenda
zaidi klabu ya Barcelona kwa sababu ya staili yao ya uchezaji.
Aota kuisaidia Tanzania
Nick
(pichani), ambaye ni chotara anayetokana na mzazi wa Kijerumani na
Kitanzania, anasema akikua na kuwa mchezaji mkubwa kama anavyoota,
atatumia sehemu ya fedha atakazopata kusaidia mambo mbalimbali nchini,
hasa hasa tatizo la umeme na kusaidia watoto walio kwenye mazingira
magumu. (CHANZO: MWANANCHI) (FS)
0 comments:
Post a Comment