Staa wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi akiwa kwenye mahaba mazito na boyfriend wake aitwaye Hunter Sleiyum.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Snura aliwataka wanaume wakware
waache kumsumbua kwa sababu amempata mwanaume sahihi maishani mwake,
anafurahia mapenzi na uzuri zaidi mpenzi wake anampenda yeye pamoja na
mwanaye.
Snura Mushi akiwa na Hunter Sleiyum.
“Hata kuamua kufanya kazi hii ya kunengua majukwaani ni kwa sababu
nilikwepa mambo ya kujiuza kwa wanaume, kazi hiyo siiwezi kabisa, niko
tofauti na wengine wanaokubali kujiuza na kutothamini miili yao,”
alisema Snura.Mbali na kumzungumzia mpenzi wake huyo ambaye ni DJ wa Maisha Club, Snura alikanusha kuhusu taarifa za kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngasa.
“Huwezi kuamini, Ngasa hajawahi kutoka na mimi, alikuwa ni mshkaji tu,” alisema Snura.
0 comments:
Post a Comment