Gari ya wagonjwa toka Ileje ikiingia Hospitali ya rufaq Mbeya
Majirani wakimuhudumia majeruhi NA Ezekiel Kamanga,Ileje Mbeya- Mbeya Yetu Blog.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la London
Haonga(61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya Mbebe Wilaya ya Ileje
Mkoani Mbeya amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa nyeti zake na watu watatu
wasiofahamika kisha kutokomea nazo kusikojulikana.
Tukio
hilo limetokea majira ya saa mbili usiku April 19 mwaka huu baada ya
mmoja kati ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee huyo kisha kubisha
mlango akiomba msaada wa kuonyeshwa njia akidai amepotea njia.
Mzee
London alipotoka nje ya nyumba akiwa anamwelekeza njia mtu huyo
anayedaiwa kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka nyumbani kwake
alifunikwa na kitambaa usoni na watu wawili kisha kuangushwa na kukatwa
nyeti zake ambazo waliondoka nazo.
Mtendaji
wa Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga amesema baada ya unyama huo Mzee
London alipoteza fahamu na alipozinduka alipiga yowe kuomba msaada
ambapo majirani walifika na kutoa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya
Wilaya ya Ileje huku wakiwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.
Kwa
mujibu wa Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa watuhumiwa wa tukio hilo
wanatokea Mpemba wilaya ya Momba ambao walitambuliwa na mhanga wa tukio
hilo ambapo baada ya kupewa PF 3 mzee London amekimbizwa Hospitali ya
Rufaa Mbeya ambapo alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa 11:00
jioni April 20 huku akilalamika kwa maumivu makali.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo cha awali imedaiwa sababu za
kutendewa ukatili huo umetokana na mmoja wa ndugu aliyedai kuwa mzee
huyo anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mdogo wake
hivyo watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.
Aidha
imedaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine kudai kuwa tukio
hilo kuhusishwa na imani za kishirikina kwani imedaiwa watuhumiwa
kuimbilia nchi jirani mara baada ya kutenda kitendo hicho cha kikatili.
Kamanda
Msangi ameoa wito kwa jamii kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi
amesema pindi wanapokuwa na migogoro ni vema kutatua migogoro kwa njia
ya mazungumzo ili kuleta amani na kuahidi wale wote waliohusika na tukio
hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwani hakuna mtu
aliye juu ya sheria.
0 comments:
Post a Comment