Wednesday, 12 October 2016

Burundi imeamua kusitisha ushirikiano wake na UN kuhusu Haki za Binadamu

...
Serikali ya Burundi imechukua uamuzi wa kusitisha ushirikiano wake na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, inayotuhumiwa kula njama katika kuandaa ripoti ya Uchunguzi Huru wa Umoja wa Mataifa (EINUB).

"Kufuatia njama ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu nchini Burundi, katika maandalizi ya ripoti ya uongo na yenye utata ya Wataalam wanaodaiwa kufanya Uchunguzi Huru wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi (EINUB), Serikali ya Burundi imeamua kusitisha ushirikiano wowote na kushirikiana katika miundo yake yote, pamoja na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binanadamu hadi itakapotangazwa tena." Maneno haya yameonekana kwenye tangazo lililosainiwa Jumanne hii Oktoba 11, 2016 na Philippe Nzobonariba, katibu Dola na Msemaji wa serikali.

Kwa mujibu wa tangazo hili, uamuzi huo ulifahamishwa maofisa wa Ofisi hii wakati wa kikao cha kazi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Burundi Alain Aimé Nyamitwe, Jumatatu hii, Oktoba 10, 2016.
"Kwa maana hii, Burundi inaomba kwa kusubiri, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kuteua timu itakayoendesha mazungumzo kuhusu makubaliano ya makao makuu, ambayo yataweka wazi majukumu yake, muda na idadi ya wafanyakazi wake nchini Burundi," imeongeza taarifa hiyo.
Uamuzi huu unakuja baada ya maandamano mjini Bujumbura mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya makao makuu ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ambapo waandamanaji waliomba ofisi hiyo kufungwa haraka iwezekanavyo.

Ripoti ya EINUB ilikuwa chanzo cha azimio HRC33 lililochukuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo linaomba kuundwa kwa Tume ya Kimataifa ya Uchunguzi wa ukiukaji wa haki zabinadammu nchini Burundi.Azimio ambalo lilikataliwa na serikali ya Burundi, ambayo inautuhumu Umoja wa Ulaya kuwa imeandaa na kupanga njama dhidi yake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger