Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU
imetoa muda wa siku 3 kwaajili ya wanafunzi zaidi ya 4000 ambao wamekosa
fursa ya kudahiliwa katika hawamu tatu za udahili zilizofanywa na tume
hiyo
Kaimu mkurugenzi wa udahili na
nyaraka wa TCU Dkt. Kokuberwa Mollel amesema udahili huo utaanza tarehe
24 hadi tarehe 26 mwezi huu kwaajili ya kozi mbalimbali ambazo bado
hazijajazwa kwani tayari udahili umekamilika kwa wanafunzi wanaosomea
masomo ya udaktari ambapo Jumla ya wanafunzi zaidi ya 2000 wamechaguliwa
kati ya wanafunzi zaidi ya 10,000 waliotuma maombi yao
Dkt. Kokuberwa amesema wanafunzi
wengi walioachwa kwenye usajili wameshindwa kutofautisha viwango vya
ufaulu wao na vigezo vya vyuo husika hivyo wameaswa kuchagua kozi
watakazo zikuta katika tume hiyo na kuacha kung'ang'ania kozi ambazo
hawajakidhi vigezo vyake.
0 comments:
Post a Comment