Baada ya Rais John Magufuli kuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda kumaliza tofauti zao vinginevyo atawaondoa, Kigwangalla ameibuka na kudai kuwa tayari walishamaliza tofauti zao na sasa hali ni shwari.
Kupitia akaunti yake ya Twitter na Instagram amesema walishafanya kikao na Katibu Mkuu, Prof. Adolf Mkenda cha kumaliza tofauti zao.
“Kazi ya Urais ni ngumu sana, tulioteuliwa na Rais kumsaidia utendaji/usimamizi wa maeneo mbalimbali hatupaswi kumuongezea frustrations nyingine zaidi, sisi kwenye Wizara yetu, baada ya kikao na Chief Secretary tulimaliza tofauti zilizokuwepo na sasa hali ni shwari,” amesema Kigwangalla.
Ni imani na heshima kubwa sana kwako kuteuliwa kuwa Waziri kwenye nchi yako. Kwenye nchi ya watu milioni 60, kwa nini Hamisi KIGWANGALLA? Sijui. Ni neema na baraka za Mungu tu. Maana siyo kila mtu kwenye maisha yake atapata fursa ya kuhudumu kwenye serikali kama Waziri ama kama Katibu Mkuu kwenye serikali. Siibezi wala siwezi kuichezea fursa hii adhimu.
Ni kwa kuelewa ukweli huu na ushauri, mwongozo na maelekezo ya wakuu wa kazi, na watendaji wazoefu kwenye utumishi wa umma, kama Katibu Mkuu Kiongozi, tulikaa mimi na Katibu Mkuu wangu na kukubaliana kufungua ukurasa mpya wa mahusiano mazuri zaidi kwa manufaa ya nchi yetu.
Kuondolewa kwenye nafasi ya Uwaziri unaweza kuondolewa kwa sababu mbalimbali lakini kuondolewa kwa sababu watu wazima, tena viongozi, ambao mmepewa fursa ya kushauriwa, mmeshindwa kuelewana, ni upumbavu! Mimi siyo mpumbavu.
Kuleta kiburi na jeuri kwenye mazingira Haya ni upumbavu. Kwanza sisi waislam tunafundishwa kuwa wanyenyekevu, maana ‘kiburi’ ni sifa ya Mungu, siyo yetu wanadamu. Kufanya kiburi na jeuri ni upumbavu. Hekima ya Mungu ni kujishusha na kumshinda shetani.
Sina jeuri wala kiburi sababu nimelelewa vizuri na bibi yangu Mama Bagaile, na pia naogopa hasira za Mungu. Tumalizie haya masaa kwa amani! Happy New Year Good People. Nitaendelea kutoa darasa la mambo niliyojifunza 2019, na mipango yangu ya 2020.
Nipo jimboni nachunga ng’ombe wangu kidogo. Ningekuwa Dar ningemtembelea Prof. Mkenda kwa ajili ya picha tukigonga glass ili mjue tuko sawa 😀. Mhe. Rais yeye ana namna yake ya kupata taarifa zetu. Atazipata tu! 😀. Limeisha hilo au niongeze volume? 🤷🏾♂️ Wakatabahu Dkt. Hamisi KIGWANGALLA, MB., MNEC, WMU.
0 comments:
Post a Comment