Tuesday 28 January 2020

Kocha wa Yanga achukizwa na mbwembwe za Morrison..... ''Kitendo alichofanya ni kuwakosea heshima wapinzani''

...
Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Luc Eymael amesema hapendi kuona mchezaji wake, kiungo Bernard Morrison akiwadhalilisha wapinzani wake kwa staili yake ya uchezaji.

Kauli hiyo ameitoa  Januari 26, 2020 baada ya kumalizika kwa mchezo wake na Timu ya Tanzania Prisons katika  Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federation Cup (ASFC)' ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa 2-0,

Kocha Eymael amesema kuwa ameshaoongea na mchezaji huyo juu ya aina yake ya mchezo ambao unawadhalilisha wapinzani.

"Mimi sipendezwi kuona mtu anawadhalilisha wengine, ukifanya vile Ulaya utafanyiwa 'tackle' ya hatari sana. Ukiangalia Liverpool, Mo Salah anaweza kufanya hivi?, Sadio Mane anafanya hivi? hapana na mimi nimeshaongea na Morrison nimemwambia sipendi staili hii", amesema Eymael na kuongeza kuwa;

"Mashabiki wanapenda kuona mchezaji akifanya hivyo lakini kwangu mimi ni kutowaheshimu wapinzani na nimeshamwambia Bernard Morrison",

Katika michezo miwili ya Yanga, Morrison ametokea kupendwa na mashabiki wa klabu hiyo kutokana na aina ya uchezaji wake uliojaa mbwembwe za kupanda juu ya mpira huku mashabiki wa timu hiyo wakimpa sifa lukuki na kudai Morrison ni wakina Chama 500 (Chama ni mchezaji wa Simba).


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger