Friday, 31 January 2020

Serikali Yasema Mkopo wa Benki ya Dunia wa Dola za Marekani Milioni 500 kwa nchi ya Tanzania haujasitishwa bali majadiliano yanaendelea.

...
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbasi amewatoa hofu Watanzania kuhusu madai kuwa Benki ya Dunia (WB) imesitisha kutoa mkopo wa masharti nafuu wa Dola 500 milioni za Kimarekani kwa Tanzania, akibainisha kuwa bado wapo kwenye mazungumzo.

Ameeleza hayo jana Alhamisi Januari 30, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Dk Abbasi ameeleza hayo baada ya kikao cha bodi ya utendaji ya Benki ya Dunia ambacho kingetoa uamuzi kuhusu kuruhusu mkopo huo kuripotiwa kuahirishwa.
 
Kikao hicho kilipangwa kufanyika Jumanne Januari 28, 2020  kwa ajili ya kuidhinisha mkopo huo, lakini kikaahirishwa dakika za mwisho kutokana na kile kilichoripotiwa na vyombo vya habari vya nje kuwa ni ombi la taasisi ya kijamii ambayo ina wanachama wake Tanzania.

Kabla ya kuahirishwa kwa kikao hicho, mkurugenzi anayehusika na haki za watoto wa taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na haki za binadamu ya Human Rights Watch (HRW), Zama Neff aliiomba WB kuchelewesha fedha hizo hadi suala la wasichana wanaopata mimba shuleni litakapopatiwa ufumbuzi kuhusu mustakabali wa elimu yao.

Katika maelezo yake , Dk Abbasi amesema, “walipanga kukutana siku fulani, mmoja wa wawakilishi wao aliomba wakutane leo,  mtu anatoka hapo mishipa imekutoka eti mkopo umesitishwa,sio kweli.... kukopa unaweza kuomba benki moja ukakosa nyingine ikakubali kwa hiyo ni majadiliano yanaendelea.”

==>>Msikilize hapo chini


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger