Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dk Medard Kalemani ametoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kuhakikisha anafuatilia gharama za umeme zinazotozwa kwa wananchi wa kisiwa cha Ukerewe mkoani humo.
Imeelezwa leo bungeni kuwa Watumiaji wa umeme katika Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza wanatumia nishati hiyo kwa gharama ya Sh2,500 kwa uniti moja badala ya Sh100 inayotozwa kwa maeneo mengine.
Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma leo na Mbunge wa Ukerewe (CCM), Joseph Mkundi wakati akiuliza swali la nyongeza akiitaka Serikali kuchukua hatua.
Akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema jambo hilo halikubariki.
Dk Kalemani amesema Mtanzania yeyote anayetumia umeme usiozidi uniti 70 kwa mwezi, anapaswa kulipia kiwango cha Sh100 kwa uniti siyo gharama ya huko.

0 comments:
Post a Comment