Saturday 30 November 2019

Picha : SHIRIKA LA FIKRA MPYA LAENDESHA KONGAMANO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

...



Shirika lisilo la kiserikali liitawalo Fikra Mpya la Mkoani Shinyanga, linalofanya shughuli ya kutoa elimu ya kujitambua kwa mtoto wa kike, limeendesha Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike kutoka Shule za Sekondari Nane Mjini Shinyanga.


Kongamano hilo limefanyika leo Novemba 30, 2019, kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu mjini Shinyanga (Shycom), na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, wakiwemo maofisa ustawi jamii, maendeleo, dawati la jinsia kutoka polisi, walimu, pamoja na wazazi.

Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah, amesema wameendesha Kongamano hilo kwa wanafunzi wa kike, ili kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwemo kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni, ambalo limekuwa likizima ndoto za wanafunzi walio wengi.

Amesema wameendesha Kongamano hilo kama sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia, ambayo ilianza kuadhimishwa Novemba 25 mwaka huu na itahitimishwa Desemba 10, kwa kufanya mijadala mbalimbali ya kujadili namna ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake.

“Shirika letu tumeamua kuendesha Kongamano hili la kupinga vitendo ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ambapo tunajadili kwa pamoja na wanafunzi ili kupata suluhu ya kutokomeza ukatili na wanafunzi wapate kutimiza ndoto zao,” amesema Josiah.

“Mkoa wetu wa Shinyanga na Kanda ya ziwa inatajwa kuongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake, ambapo takwimu zinaonyesha kuanzia Januari hadi Juni 2019 kanda ya ziwa inaongoza kwa asilimia 38, ikifuatiwa na mikoa ya nyanda juu kusini asilimia 32, Pwani asilimia Tisa (9),

“Kanda ya kaskazini asilimia Tisa (9), Kanda ya Kati asilimia Saba (7), pamoja na Kanda ya Magharibi asilimia Tano (5),”ameeleza Josiah.

Naye mgeni Rasmi kwenye Kongamano hilo Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda, akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wanafunzi wanapokuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili wasikae kimya, bali watoe taarifa ili wahusika wapate kuchukuliwa hatua na kukomesha vitendo hivyo.

Nao baadhi ya wanafunzi akiwemo Mariamu Charles kutoka Shule ya Sekondari Mwasele, wameshukuru kuendeshwa kwa Kongamano hilo, ambalo wamedai limewasaidia kuwapatia upeo namna ya kupinga vitendo ya ukatili wa kijinsia, pamoja na wapi pa kwenda kutoa taarifa hizo.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Mkoani Shinyanga Leah Josiah akizungumza kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia leo Jumamosi Novemba 30,2019. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Mkoani Shinyanga Leah Josiah akizungumza kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Mgeni Rasmi Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Kongamano la Kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wageni waalikwa wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Mratibu kutoka Shirika la Women Fund Tanzania Mkoani Shinyanga Glory Mbia, akifungua mjadala wa kujadili juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutafuta suluhu ya kuvitokomeza.

Mwenyekiti wa baraza la watoto manispaa ya Shinyanga Rose Matiku akichangia mada kwenye Kongamano hilo la kupinga ukatili wa kijinsia.

Afisa wa Jeshi la Polisi kutoka dawati la Jinsia wilaya ya Shinyanga Joseph Christopher, akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah.

Mzazi Aida Luben akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Mwandishi wa habari Isack Edward kutoka Radio Faraja, akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia namna vyombo vya habari vinavyosaidia kutoa elimu ya kutokomeza matukio hayo.

Mwanafunzi Verynice Busanga kutoka Shule ya Sekondari Mwasele, akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Mwanafunzi Mariam Charles kutoka Shule ya Sekondari Mwasele akichangia mada kwenye Kongamano hilo la kupinga ukatili wa kijinsia.

Awali wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa Kijinsia.

Mgeni Rasmi afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda akipokea maandamano kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wageni waalikwa wakiwa na mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.

Wageni waalikwa, wanafunzi pamoja na mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya ,wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia.


Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger