Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk Leonard Maboko ameeleza anavyotamani kushuhudia Serikali ikigawa kondomu bure hasa katika maeneo hatarishi ikiwemo nyumba zote wageni na kwenye baa.
Akizungumza leo Alhamisi Novemba 28, 2019 katika kongamano la kitaifa la maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani jijini Mwanza,Dkt. Maboko amesema ifike mahali hali ya kuzuia maambukizi isichukuliwe kama mzaha.
Amesema anatamani mwaka 2020 nyumba zote wageni, baa na maeneo mengine kondomu kugawiwa bure.
"Natamani mwakani tuweze kusambaza kondomu kila mahali ili tuweze kudhibiti ugonjwa huu, najua huko ndiko watu wanakutana na kufanya wanavyofanya lakini kama Serikali tuone namna gani tunawasaidia wale wanaoshindwa kununua," amesema Dk. Maboko
Amesema lengo ni kuzuia maambukizi mapya ya Ukimwi kwa vijana kwa maelezo kuwa kwa sasa ndio kundi linaloongoza kwa kupata maambukizi mapya.
0 comments:
Post a Comment