Thursday 28 November 2019

Picha : AGAPE YAENDESHA KIKAO KUJADILI KUTENGENEZA MUONGOZO WA KUPAMBANA NA UKATILI SOKONI SHINYANGA

...


Shirika lisilo la kiserikali Agape Aids Control Programme limeendesha kikao cha kujadili namna ya kutengeneza muongozo ambao utatumika kwenye masoko ya Shinyanga Mjini, kwa ajili ya kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia kwenye Masoko.

Kikao hicho kimefanyika leo Novemba 28, 2019, kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Liga, ambacho kimeshirikisha viongozi wa masoko sita ya Shinyanga mjini, maofisa ustawi, maendeleo ya jamii, wanasheria, dawati la jinsia, pamoja na wajumbe wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto Mtakuwwa.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Mwansheria kutoka Shirika la Agape Felix Ngaiza, akimwakilisha mkurugenzi wa Shirika hilo John Myola, amesema, utengenezaji wa muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili kwenye masoko, utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia masokoni.

Amesema Shirika hilo limekuwa likitekeleza mradi wa kupambana na matukio ya ukatili wa kijinisa sokoni, uitwao Mpe Riziki Si Matusi, ambapo sasa wameamua watengeneze muongozo ambao utatumika kuzuia na kupambana na matukio hayo ya ukatili wa kijinsia sokoni, ili pawe mahali salama pa kufanyia biashara.

“Muongozo huu ni muhimu sana ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia masokoni, na ndio maana leo tumeamua kufanya kikao na viongozi wa masoko, maofisa ustawi jamii, maendeleo, dawati la jinsia, wanasheria, na wajumbe wa Mtakuwwa, ili tupate kuutengeneza na kuanza kutumika,”amesema Ngaiza.

Aidha amesema muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia kwenye Masoko, utakuwa ukitoa faini na adhabu mbalimbali kwa watu ambao watakuwa wakifanya matukio hayo ya ukatili kwenye masoko.

Naye Afisa mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ Helena Daudi, amesema mradi huo umeanza kutekelezwa tangu mwaka Novemba 2018 ambao unakoma mwaka huu 2019, ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kupunguza ukatili huo kwa kiwango kikubwa.

Amesema mradi huo unafadhiliwa na Shirika la UN WOMEN kupitia shirika la Equality for Growth (EFG), ambao umedhamiria kutokomeza ukatili kwenye masoko sita ya manispaa ya Shinyanga dhidi ya wanawake na wasichana, ambayo ni Kambarage, Soko kuu, Nguzonane, Ngokolo, Majengo mapya, na Ibinzamata.

Nao baadhi ya wenyeviti wa masoko akiwemo Alex Stephen kutoka soko kuu la Shinyanga, wamebainisha matukio ya ukatili ambayo yamekuwa yakitendeka ikiwamo kutolewa kwa lugha chafu za matusi ya nguoni, kushikwa maumbile kwa wanawake bila ya ridhaa yao, kutakwa kimapenzi kwa nguvu, kudhulumiwa pamoja na vipigo.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mwanasheria wa Shirila la Agape Felix Ngaiza akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kujadili namna ya kutengeneza muongozo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Afisa mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ kutoka Shirika la Agape Helena Daudi, akielezea umuhimu wa masoko kuwa na muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni, ambapo utasaidia kutokomeza ukatili huo.

Afisa mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ kutoka Shirika la Agape Helena Daudi, akielezea umuhimu wa masoko kuwa na muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni, ambapo utasaidia kutokomeza ukatili huo.

Mwanasheria kutoka Shirika la Agape Emmanuel Nyalada akiwasilisha mada kuhusu muongozo wa kuzuia na kupambana na ukatili kijinsia sokoni.

Meneja miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga Mushi Josephat akieleza kuwa muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni utasaidia kumalizana kesi wao kwa wao zinazohusu ukatili, kuliko kupelekana kwenye vyombo vya Sheria ambapo matukio yote ya ukatili ni Makosa ya Jinai.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadili utengenezaji wa muongozo ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia sokoni.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadili utengenezaji wa muongozo ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia masokoni.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadiri utengenezaji wa muongozo ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia masokoni.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Mwenyekiti wa Soko kuu la Shinyanga Alex Stephen akichangia mada kwenye kikao hicho.

Mhasibu wa Soko la Ibinzamata Juliana Francis akichangia mada kwenye kikao hicho.

Msaidizi wa kisheria kutoka Soko kuu la Shinyanga Zera Semuguruka, akichangia mada kwenye kikao hicho.

Mwakilishi wa Soko la Nguzo Nane Hilda Athanas, akichangia mada kwenye kikao.

Mchungaji wa kanisa la KKKT Makedonia Harold Mkaro, ambaye pia ni mjumbe wa MTAKUWWA, akichangia mada kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Mwenyekiti wa Soko la Kambarage Seif Mtete akiwasilisha kazi ya kikundi.

Wajumbe wakiendelea kuwasilisha kazi ya kikundi.

Wajumbe wakiwasilisha kazi ya kikundi.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger