Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Devis Deogratius akiongea na mawakala na wageni waalikwa
Mfanyabiashara Julius Masalu
mkazi wa Mwanza (katikati) akipokea funguo za gari alilojishindia
katika droo ya promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha
mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL)
kutoka kwa Meneja wa Chapa ya Konyagi,Martha Bangu (Kulia),anayeshuhudia
kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TDL,Devis Deogratius.Droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyika mwishoni
mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwishoni
mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na
kanda ya ziwa
Baadhi ya maofisa wa TDL na mawakala katika picha ya pamoja
Mawakala wa Konyagi wakiserebuka wakati wa hafla hiyo
Meneja Masoko wa TDL,George Kavishe akiwashukuru mawakala walioshiriki kwenye promosheni hiyo
Mfanyabiashara Julius Masalu (58) mkazi wa Mwanza ameibuka mshidi wa gari aina ya Eicher lenye thamani ya shilingi milioni 56 katika mzunguko wa pili wa bahati nasibu ya Promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL).
Droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyika katika
viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwihoni mwa wiki ikihusisha
washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa na
kusimamiwa na afisa wa Bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha Humudi
Abdul Hussein.
Akiongea
kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Masalu alisema ametoka
Mwanza akiamini kuwa atajishindia gari hilo na kwamba bahati nasibu hiyo
imeendeshwa kwa uwazi na hakuna upendeleo unaoweza kufanyika.
“Katika bahati nasibu hii hakuna longo
longo,shindano limeendeshwa kwa uwazi mkubwa sana na namshukuru Mungu
kwa kuweza kupata zawadi hii ya gari itanisaidia sana katika kusambaza
bidhaa zakampuni ya konyagi kwa wateja wangu,” alisema Masalu.
Kaimu Meneja Mkuu wa Konyagi, Devis Deogratius alisema dhumuni ya promosheni hiyo ni kukuza
uhusiano wa kibiashara na wasambazaji wa bidhaa za TDL pamoja na
kuwapatia kifaa kitakachosaidia katika kupanua masoko ,kusambaza na
kuongeza ufanisi.
“Safari
ilianza mwezi wa saba hadi mwezi wa tisa ,kumekuwa na usawa katika
mchakato huu wa kumpata mshindi na hakuna upendeleo wowote ,wale ambao
wamefikia malengo wamefika katika promosheni hii na kuwepo hali ya usawa katika kushinda zawadi ya gari”alisema Deogratius.Alisema mbali na mshindi huyo wa gari katika droo hii ya kwanza washiriki watano walibahatika kujishindia katoni 10 za Konyagi kila mmoja.
Baadhi ya washiriki katika droo hiyo, Mkamba Zephania na Joas Muganyizi walisema wameridhishwa na mchakato mzima ulivyofanyika katika kuchezesha droo na wala hapakuwa na kasoro ama udanganyifu wowote.
“Kampuni ya TDL kupitia bidhaa yake ya Konyagi katika promosheni ya Nunua Uza,Shinda
na Konyagi imesaidia kuwakutanisha wafanyabiashara wa maeneo mengine ya
kanda ya Kaskazini na kanda ya ziwa hali inayochangia kuongeza wigo
katika kufanya biashara”.Alisema Muganyizi.
Washindi
wengine waliojinyakulia katoni 10 kila mmoja za bidhaa ya Konyagi na
maeneo wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Linus Mathew (Kagera) Msemo
Enterprises (Arusha) ,Joace Muganyizi(Bukoba) Mkamba Zephania (Bariadi)
na Yohana Masunga (Geita).
Huu
ni mzunguko wa pili wa droo ya bahati nasibu ya Promosheni ya Nunua
Uza,shinda na Konyagi ambapo katika droo ya kwanza mfanyabiashara Grace
Oroki, mkazi
wa Jijini Dar es salaam, alijinyakulia gari kwa mawakala wa kuuza
bidhaa za kampuni ya TDL wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini na Pwani.
0 comments:
Post a Comment