Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabir Bakari
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imesema Kuna tatizo la Mfumo wa Mawasiliano ya Intaneti kwenye Mkongo wa Baharini.
Kama umekosa huduma ya intaneti kwa saa kadhaa leo, tambua shida sio kifaa unachotumia bali ni tatizo la kiufundi lililotokea kwenye miundombinu ya intaneti iliyopitishwa baharini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabir Bakari amelithibitisha hilo alipotafutwa na Mwananchi Digital leo Jumapili Mei 12, 2024.
"Kunaonekana kuna tatizo la kiufundi kidogo linalohusiana na 'marine cables' kwa hiyo tunajaribu kupata maelezo zaidi," amesema Dk Bakari.
Dk Bakari amesema kwa sasa wanaangalia namna ya kupata taarifa zaidi ili kujua ilipo changamoto ili kuchukua hatua.
Tatizo la mtandao wa intaneti limeanza tangu saa 5 asubuhi.
0 comments:
Post a Comment