Na Oscar Assenga,Tanga
CHUO cha Bahari cha Jijini Dar es Salaam(DMI) kimeshiriki maonyesho ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu Jijini Tanga huku wakijivunia kutoa wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kusanifu na kuzikarabati meli kupitia Temesa na hivyo kuondoa uhaba uliokuwepo awali nchini .
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Banda lao lililopo eneo la Shule ya Sekondari Popatlaly kunakofanyika maadhimisho ya elimu,ujuzi na ubunifu Captain Mohamed Kauli alisema wameshirika kwa lengo la kueleza wanachokifanya ikiwemo ufanisi wa meli,usafirisha majini,utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini,usanifu ini na ujenzi wa meli na ubaharia.
Alisema awali chuo hicho kilikuwa kinazalisha mabaharia wakati kilipoanzishwa lakini ili kukabiliana na ombwe la ukosefu wa ajira kutokana na vijana wengi kumaliza vyuo na kukosa ajira na wahitimu haoo wanafaida kubwa mbili wanapohitimu chuo kupata ajiri nchini kwenye sekta ya usafirishaji majini na nje ya nchi kwenye meli.
“Kwa kweli tumekuwa tukizalisha idadi kubwa ya mabaharini wanaofanya kazi nje na ndani ya nchi kuna gepu kwenye utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini lakini pia gepu la upatikanaji wa meli awali zimekuwa zikiagizwa kutoka nje kwa gharama kubwa”Alisema
Alisema lakini sasa Serikali imetengeza wataalamu wanaotoka kwenye chuo hicho ambao wanajenga meli,kuzisanifu ,kuzikarabati kwenye eneo hilo serikali kupitia Temesa wanajenga na kukabarati meli hizo hapa hapa nchini.
Awali akizungumza mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,Masaka Julias alisema kwamba mafunzo ambayo wanayapata kwenye yamewawezesha kubuni vitu mbalimbali a hivyo kuwawezesha wanapomaliza kuweza kujiajiri kupitia ujuzi walioupata.
Alisema kwamba kwa sasa kupitia mafunzo hayo unawasaidia kutengeneza vitu mbalimbali vya ubunifu huku akieleza wamebuni wazo la kutengeneza mashine ya kutengeneza chilsource na ya kufunga vifuniko kwenye chupa ambayo inasahisisha.
0 comments:
Post a Comment