Monday, 15 August 2022

RAIS WA FEMATA JOHN BINA ATEMBELEA BANDA LA WANAWAKE WACHIMBAJI MADINI 'TAWOMA' ... AKEMEA UTOROSHAJI WA MADINI

...
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina (wa pili kushoto) akiwa katika banda la Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) katika uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) , Rachel Njau (katikati) akimwelezea Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina (wa pili kulia) kuhusu shughuli zinazofanywa na TAWOMA 

Na Mwandishi wetu - Shinyanga
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza wakati akitembelea mabanda ya washiriki wa madini Marathon Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga.


Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina amelaani vitendo vya Utoroshaji madini na kuwaonya baadhi ya wachimbaji wa madini wanaotorosha madini na baadhi ya watu wanaoshiriki utoroshaji madini.


Rais huyo wa FEMATA ameyasema hayo Agosti 14,2022 wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa Madini Marathon Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika Jumapili Agosti 15,2022 katika uwanja wa CCM Kambarage Mkoa wa Shinyanga.


"Kupitia Shinyanga madini Marathon natumia nafasi hii kupongeza
kamati ya maandalizi na kulaani utoroshaji wa madini. Nawaonya
wachimbaji madini na baadhi ya watu wanaoshiriki utoroshaji madini kuacha mara moja tabia hiyo", amesema Bina.


Bina amesema Wachimbaji Wadogo wengi wao hawana mitaji ya kununua Miundo Michundo hivyo kuziomba Taasisi za Kifedha kuangalia njia nzuri ya kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini kwa kuwapatia mikopo kwani hivi sasa bado kuna ugumu katika kuwakopesha wachimbaji hao.


Pia Rais huyo wa FEMATA ametembelea banda la viongozi wa Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) na kuwapongeza kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ikiwemo kuwaunganisha wanawake wachimbaji wengine katika chama hicho.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo mkoa wa Shinyanga SHIREMA Hamza Tandiko amempongeza Rais wa FEMATA kwa kufika mkoani Shinyanga na kushiriki Shinyanga madini Marathon huku katibu wa SHIREMA Gregori Kibusi akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kuhimiza wachimbaji wa madini kulipa kodi na kuepuka kutorosha madini hali itakayo sadia kuchangia ukuaji wa pato la Taifa.
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina akiwasalimia washiriki wa madini Marathon Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger