Saturday, 27 August 2022

HUYU NDIYE RUBANI MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI ALIYEVUNJA REKODI

...

Mack Rutherford

MACK Rutherford mwenye umri wa miaka 17 raia wa Uingereza aliyekulia nchini Ubelgiji ameweka rekodi ya kuwa rubani mwenye umri mdogo zaidi kuendesha ndege ndogo pekeyake.


Awali rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na rubani Muingereza Travis Ludlow ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 na siku 150 alipoanza safari yake mwaka 2021.

Mack Rutherford raia wa Uingereza

Katika safari yake ya miezi mitano akizunguka nchi takribani 52 Mack Rutherford alitua katika mji wa Sofia huko nchini Bulgaria.



Mack anaeleza kuwa kipindi cha safari yake alikumbana na dhoruba za mchanga huko Sudan na kulala usiku kucha kwenye kisiwa cha Pasifiki kisichokaliwa na watu.

Mack Rutherford ana umri wa miaka 17

Hata hivyo dada yake mkubwa Zara anashikiria rekodi kuwa mwanamke mdogo zaidi kuendesha ndege peke yake duniani kote.


Imeandaliwa na Simon Molanga kwa msaada wa mtandao.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger