Sunday, 28 August 2022

MAMA AFUNGIWA CHUMBANI NA MWANAE AKIDAIWA ELFU 7 NA MWENYE NYUMBA SHINYANGA MJINI

...

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi Adam akizungumza na Mariam Hamis  kupitia dirishani akiwa amefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela 
Kulia ni Mariam Hamis  akizungumza kupitia dirishani akiwa amefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela 
Mlango wa chumba cha Mariam Hamis ukiwa umefungwa na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela huku yeye akiwa ndani

Zoezi la kuvunja kufuli kwenye Mlango wa chumba cha Mariam Hamis uliofungwa na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela likiendelea
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi Adam akifungua mlango wa Mariam Hamis  aliyefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela 
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi (kushoto) akizungumza na Mariam Hamis  aliyefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwanamke aitwaye Mariam Hamis mkazi wa mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga amefungiwa ndani ya chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela takribani saa 10 hadi serikali ya mtaa ilipofika kuvunja mlango kutokana na kile kilichoelezwa kuwa anadaiwa shilingi Elfu saba na mia nne (7400) ya bili ya maji.


Mariam Hamis amefanyiwa ukatili wa kufungiwa ndani ya chumba chake tangu jana Jumamosi majira ya saa tano usiku mpaka leo asubuhi saa tatu asubuhi wajumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi walipopata taarifa kuhusu tukio hilo na kufika nyumbani kwake na kulazimika kuvunja kufuli lililofungwa na mwenye nyumba aliyopanga aliyejulikana kwa jina la Evodia Charles Mahela.

Wajumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mabambasi wakiongozwa na Abdi Adam wamesema wamelazimika kuvunja kufuli hilo kutokana na kwamba kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki za binadamu.


Akielezea kuhusu kisa hicho, Mariam amesema ameshangaa kuona mama mwenye nyumba anafunga chumba hicho kwa madai kwamba hajalipa bili ya maji shilingi 7,400/=.


“Wapangaji tupo wanne,kila mpangaji anadaiwa shilingi 7400, mmoja amelipa bili ya maji, watatu hatujalipa bili ya maji lakini nashangaa mimi nimefungiwa nyumba. Humu ndani naishi na mtoto wangu mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu. Kanifungia mlango kwa kufuli tangu jana saa tano usiku, hiki chumba hakina choo ndani”,ameeleza Mariam.

Malunde 1 blog imemtafuta Evodia Charles Mahela ambaye kwa kujiamini amesema amemfungia mpangaji wake kutokana na kwamba alitaka kutoroka na pesa.

“Alikuwa anataka kutoroka na pesa,nikawaambia wafunge mpaka nitakapokuja,nikampigia simu huo usiku nikamwambia akitaka kuondoka atoe pesa au aache kitu maana wamekuwa na tabia ya kuondoka bila kulipa halafu mimi nabaki na madeni,sasa namwambia anaanza kunijibu vibaya na alikuwa anatoroka anatoroka na deni sasa mimi nitakuwa wa kulipa madeni ya watu..na geti jana usiku alilifunga funguo akakaa nazo yeye kwamba usiku huo atoroke.

“Nimeomba kufuli kwa mmoja wa wapangaji nikafunga nikawaambia asubuhi nichukue kitu chochote atoe hela, wameshahama wawili na hela na kwanini atoroke? Kwani asiage?”,amesema 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger