Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka shirika la maendeleo ya Petrol Nchini Anamaria Simoni
Na Mwamvita Issa na Neema Sawaka - Kahama
MRADI mkubwa wa Bomba la Mafuta ghafi (EACOP) kutoka Nchini Uganda kwenda Tanga unatazamiwa kuwalipa wananchi walio karibu na mradi unapopita kiasi cha shilingi bilioni 25 kama fidia ya maeneo yao kupisha ujenzi wake.
Mradi huo ambao utapita katika mikoa nane iliyopo Tanzania , Wilaya 24, Kata 134 ambapo utandazaji wa mabomba yake unatazamiwa kuwa wa kilometa 1443 kutoka nchini Uganda hadi Mkoani Tanga Nchini Tanzania.
Hayo yalisemwa jana na Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka shirika la maendeleo ya Petrol Nchini Anamaria Simoni wakati akiongea na Wafanyabiashara wa Wilaya ya Kahama juu ya fursa ambazo zitakuwa rafiki kwao wakati ujenzi wa mradi huo uifanyika.
Simoni alisema kuwa katika Wilaya ya Kahama ambapo Bomba hilo litapita kwa umbali wa kilometa 54, Wafanyabiashara wanaweza kupata fursa ya kuangalia mazingira mazuri ya kufanya shughuli za kiujasilimali katika eneo husika.
Alisema kuwa bomba hilo lina uwezo wa kusafirisha jumla ya mapipa 216,000 kwa siku huku ujenzi wake ukigharimu kiasi cha dola za kimarekani bilioni 3.5 sawa na trilioni nane fedha za kitanzania.
Akizungumzika kuhusu EACOP, Simon ambaye ndiye mkandarasi Mkuu,alisema kuwa Kampuni hiyo inaundwa na makampuni manne ambayo yenye hisa ambayo ni Shirika la Maendeleo ya Petrol Nchini (TPDC) yenye asilimia 15, Kampuni ya Total kutoka Nchini ufaransa asilimia 65, UNOC asilimia 15 pamoja na Kampuni ya CNOOC yenye asilimia 8.
Aidha alisema kuwa katika kuelekea ujenzi wa mradi huo hatua iliyopo kwa sasa ni ile ya uchukuaji wa ardhi kutoka kwa wananchi huku akiongeza kuwa Bomba hilo litafanya kazi kwa muda wa miaka 25na jumla ya wananchi 607 watalipwa fidia katika kata nane zilizopo katika Wilaya ya Kahama.
Kwa upande wake Mhandisi kutoka katika mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kutoka makao makuu Dodoma Nyaso Makwaya alisema kuwa kwa sasa ni bora kwa wamiliki wa makampuni ya wazawa kusajili kampuni zao ili waweze kupata fursa ya kufanya biashara na mradi huo.
Alisema kuwa hadi kufikia mwezi agust 31 mwaka 2021 jumla ya makampuni 852 yaliweza kusajiliwa na mamlaka hiyo na kuongeza kuwa katika makampuni ya mafuta wameayaambia kutumia bidhaa zinazotoka hapa hapa nchini.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaham a Festo Kiswaga alisema kuwa wafanyabiashara walipo katika Wilaya ya Kahama wanapoitwa katika vikao vinavyohusu fursa ni bora wakajitokeza kwa lengo la kupata maarifa na kuongeza kuwa mradi huo ni mkubwa na utawanufaisha.
Aliwataka wafanyabiashara kuungana ili waweze kuupokea mradi huo na kufanya kazi naoi li kuongeza mitaji yao na kuongeza kuwa muda umefika sasa kukaa chini na kuona jinsi gani ya wao wataweza kukidhi vigezo na kupata fursa hiyo.
0 comments:
Post a Comment