Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa serikali za mitaa kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 kwa wananchi.
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi hao kutotumia mabavu katika utoaji wa chanjo bali kuwaelimisha wananchi wapate chanjo kwa hiari.
Rais ametoa kauli hiyo leo Septemba 27, 2021wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya serikali za mitaa- ALAT Taifa Mkoani Dodoma.
“Tulisema hili jambo ni la hiari, ukipita nyumba kwa nyumba anayetaka mchome asiyetaka usichome Lakini kubwa ninalotaka kusema mtu ana hiyari ya kukubali au kukataa na kama ana elimu ya kutosha ,hawezi kukataa”
Katika mkutano huo maalum Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi hao kushirikiana na kuondoa tofauti Zao ambazo nyingi hutokana na maslahi binafsi.
0 comments:
Post a Comment