China imetangaza vikwazo dhidi ya Wamarekani wawili, raia mmoja wa Canada na Shirika la kutetea haki ili kujibu vikwazo vilivyowekwa mapema wiki hii juu ya inavyoshughulikia jamii ya Uyghurs.
Wizara ya mambo ya nje ya China imewakataza, wajumbe wawili wa Tume ya Kimataifa ya Uhuru wa Kidini ya Marekani, Gayle Manchin na Tony Perkins, Mbunge wa Canada Michael Chong na Kamati ya Bunge ya Canada ya haki za binadamu kuingia China Bara, Hong Kong na Macau.
Maafisa hao pia wamepigwa marufuku kufanya biashara na taasisi au raia wa China.
Wizara ya mambo ya nje ya China imeishutumu Marekani na Canada kwa kuweka vikwazo kulingana na uvumi na habari ghushi.
DW
0 comments:
Post a Comment