Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi |
BALOZI wa Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Nancy Sumary katika akiwa na baadhi ya watalii wengine wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani
BALOZI wa Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Nancy Sumary ametembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro huku akiwahimiza watanzania kujenga mazoea ya kutembelea hifadhi zilizopo hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio vilivyopo na kujifunza mambo mbalimbali ya uhifadhi wa wanyama pori.
Nancy ambaye aliwahi kuwa Miss Tanzania 2005 na mrembo wa Dunia Afrika mwaka huo aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa nchini iliyofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na kuzinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule.
Alisema kwamba utalii wa ndani ni jambo muhimu sana kwa watanzania kwani unamuwezesha kutumia muda mchache kuweza kujifunza na kujionea vivutio vilivyopo ndani ya nchi na kuweza kuvifurahia.
“Kwa kweli niwashukuru wananchi, Mkuu wa wilaya ya Same na Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kwa kutukaribisha mimi na familia yangu kutembelea na kufurahia utalii wa ndani ni jambo nzuri na la kipekee sana hivyo niendelee kuwasihi watanzania tutembelee hifadhi zetu”Alisema
Hata hivyo aliwakaribisha marafiki na watanzania wengine kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kwani ni eneo ambalo la kipekee kutokana na kusheheni idadi kubwa ya wanyama wakubwa na ndege ambao wageni wanakutana nao wakati tu wanapoingia kwenye eneo la lango la geti hilo.
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel Mtui alisema kwamba katika kampeni hiyo wageni ambao walijiandikisha kuingia ndani ya hifadhi ni 78 ambao kati yao kutoka wilaya ya Mwanga ni 13, Same ni 55 na Hedaru ni 10 hivyo hiyo ni idadi kubwa ya kutosha na wanategemea waliokuja watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao.
Alisema anaimani idadi kubwa ya watalii wa ndani itazidi kuongezeka zaidi kwani wageni waliotembelea hifadhi hiyo wataenda kuwaarifu wenzao huku wageni ambao walipata fursa ya kutembelea hifadhi hiyo wakipiga picha na Balozi Nancy.
“Hivyo niendelee kuwahimiza watanzania kuendelea kutembelea vivutio vya utalii ambao vipo hapa nchini ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ambayo inavuvutio vya kipekee”Alisema
Awali akizungumza wakati wa kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule alkiwakaribisha Balozi huyo na familia yake na wananchi ambao tayari walianza kujitokeza kwenye kufanya utalii wa ndani kwani wana matarajio makubwa sana na hifadhi ya mkomazi kutokana na kuwa na vuvutio vingi vinavyopatikana na vya kipelee ambavyo havipatikana maeneo mengine.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba wanatagemea hifadhi ya Taifa ya mkomozi inayokuwa kwa haraka kwa kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ikiwemo kuongeza mapato na kukuza uchumi wa serikali na mwananchi mmoja mmoja.
“Tunaweka nguvu nyingi kama serikali kuhakikisha mkomazi inakuwa na kupata miundombinu na vitu vyengine vitakavyofanya watalii kuvutiw lakini pia ujio wa faru ni kuvutio ambacho kitakuwa hakuna eneo jengine Tanzania hadi ya mkomazi kunajengwa ukuta ambao faru watawekwa pale na upo kwenye hatua zxa mwisho za ukamilishaji”Alisema
“Kukamilika kwake utawawezesha watanzania ambao watakuwa wakifika Mkomazi anakuwa na uhakika wa kuona faru na itakuwa hifadhi pekee kwenye nchi ya Tanzania na nchi chache za Afrika na wanategemea jambo hilo litasaidia kupata idadi kubwa ya wageni “Alisema Dc huyo.
0 comments:
Post a Comment