Thursday 28 March 2019

WANANCHI NJOMBE WAFURAHIA ZAHANATI YAO KUKAMILIKA

...
Na Amiri kilagalila

Wananchi wa mitaa ya Sido na Buguruni kata ya Njombe mjini mkoani Njombe,wamefurahishwa na mwenendo wa ujenzi wa zahanati ya mitaa hiyo ulionza mwaka 2012 na kushindwa kukamilika mpaka sasa kutokana na changamoto ya kamati ya ujenzi iliyokuwepo awali.

Baadhi ya wananchi wa mitaa hiyo wakizungumza na mtandao huu wamesema kuwa kwa sasa wanaridhishwa na ujenzi huo kutokana na kufikia hatua za mwisho za ukamilishaji kwakuwa tangu mwaka 2012 wamekuwa wakitoa michango yao kwa kushirikiana na wadau wengine lakini ilishindwa kukamilika kwa wakati.

“Zahanati yetu kwa sasa naona inaenda vizuri ingawa kipindi cha nyuma tumeenda kwa migogoro mingi kutokana na kamati ya nyuma kuto kufanya kazi kikamilifu hali ambayo ilikuwa ikiwakatisha tama wananchi kuendelea kutoa michango ila kwa kweli kwa sasa toka ianze kamati mpya miaka miwili hii  kweli imefika pazuri”alisema Bakari ally gohage mmoja wa wananchi waliozungumza na mtandao huu.

NOLASCO KILASI  ni mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo amesema licha ya kusua sua kwa ujenzi  katika kipindi kilicho pita lakini kamati ya sasa imeendelea na jitihada za kuhakikisha zahanati hiyo inakamilishwa huku akiwataka wananchi kuhudhuria katika mikutano yao ili kujua mapato na matumizi ya pesa zinazotumika katika ujenzi.

“kamati yetu ilianza miaka miwili iliyopita baada ya kupokea kamati iliyofika ikiwa imefika hatua Fulani ya ujenzi lakini na sisi tumeanzia mahali na kwa mujibu wa kamati tunajitanzua kwa kuendelea kuchangisha wananchi lakini changamoto ni kwamba wanachi wakichanga fedha hawafiki kwenye mikutano kujua maendeleo ya michango yao  na matokeo yao huamini mchango walioutoa unakamilisha ujenzi hata kama ni mdogo basi umemaliza kazi”alisema NOLASCO KILASI

Diwani wa kata ya njombe mjini AGREY MTAMBO amesema kazi iliyobakia ni ndogo ikiwemo kuingiza maji,umeme pamoja na kichomeo  taka katika zahanati hiyo hivyo anategemea kukamilishwa ndani ya miezi michache ijayo.

“tulipofikia ni pazuri licha ya kucheleweshwa tumebakia kuingiza maji,umeme pamoja kichomea taka ambacho ni muhimu zaidi na fedha tuliyonayo ni kidogo haiwezi kutosheleza kwa kuwa halmashauri katika hatua za umaliziaji ilileta shilingi milioni 20 ambayo imefanya kazi kubwa kwa hiyo pesa inayobaki tutaendelea kuipata kwa wananchi kwa njia ya mchango mdogo ili kukamilisha zoezi”alisema diwani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe EDWIRN MWANZINGA amewataka wananchi wa mitaa hiyo kuongeza nguvu ili kukamilisha zahanati hiyo huku akikili halmashauri yake kujitahidi katika utekelezaji wa sera ya afya kuwa na zahanati katika kila kijiji.

“Ningeomba wananchi wa mitaa ya sido na buguruni wajitahidi kwa kuwa sisi katika halmashauri yetu tupo vizuri upande wa afya katika vijiji 44 ni vijiji vitatu tu visivyokuwa na zahanati”alisema MWANZINGA

Zahanati ya mitaa ya sido na buguruni inajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 110 kutokana na BOQ ya serikali lakini mpaka sasa ujenzi huo umefika kwa gharama ya shilingi milioni 89.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger