Tuesday, 26 March 2019

NSSF,MAGEREZA KUANZISHA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI MOROGORO,WATEMBELEA SHAMBA LA BAKHARESA BAGAMOYO KUJIFUNZA

...

Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio akiwa na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo,kuhusu maandalizi makubwa yanayotarajiwa kufanywa ndani ya shamba hilo ikiwemo na miundo mbinu mbalimbali namna itakavyojengwa,Uongozi wa NSSF jana Machi 25,2019 umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000.
Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna (mwenye kofia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio akiwa na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo,namna ya kuandaa shamba la miwa,upandaji mbegu na utunzaji wake. Uongozi wa NSSF umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000 .
Muonekano wa shamba la Miwa akianza kuchipua 
Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kati) walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya shamba hilo ikiwemo kujionea ujenzi wa miundo mbinu kama vile mabwawa ya maji,mabomba ya maji,barabara yote hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi makubwa yanayotarajiwa kufamywa ndani ya shamba hilo lenye ukubwa wa Ekari elfu 25,000, kushoto ni Mkuu wa Mradi wa shamba hilo,Hosein Sufiani.
Operesheni Meneja wa shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa, Narayawan Krishna (mwenye kofia) akieleza maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji ndani ya shamba hilo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio alieongozana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo. Uongozi wa NSSF umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000 .
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kushoto) akiwa ameongozana na Wasimamizi wa shamba hilo wakitembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa miundombinu katika shamba hilo,lililopo nje kidogo ya mji mkongwe wa Wilaya ya Bagamoyo,mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi Waandamizi wa shirika hilo,walifika Ofisini kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakharesa, Bw. Said Salim Bakharesa (pichani kulia),kumshukuru mara baada ya kumaliza ziara yao walioifanya asubuhi Machi 25,2019 ya kutembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo ya sukari.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kulia ) akimsikiliza Mkuu wa Mradi wa shamba hilo,Hosein Sufiani alipokuwa akieleza namna mbegu za miwa zinavyooteshwa ndani ya Kitalu,jana Machi 25,2019,ambapo Uongozi wa NSSF ulietembelea shamba la sukari la Bagamoyo lenye ukubwa wa Ekari 25,000 linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa  Makampuni ya Bakhresa, Bw. Said Salim Bakharesa ofisini kwake jana  Machi 25,2019 jijini Dar,akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi  waandamizi wa shirika hilo (hawapo pichani),walipokwenda kumshukuru mara baada ya kumaliza ziara yao walioifanya leo asubuhi walipotembelea  shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa kwa  lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo ya sukari. 

Serikali kupitia Shirika la Hifadhi ya Jamii, NSSF na Jeshi la Magereza  Tanzania, wapo katika hatua za mwisho za uanzishwaji wa mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Morogoro Vijijini, eneo ambalo  linamilikiwa na Jeshi la Magereza.NSSF kupitia kampuni yao tanzu ya  Mkulazi imeamua kuliendeleza shamba hilo kwa kushirikiana na Jeshi la  Magereza katika kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha sukari, lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa sukari nchini, pia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni za kuagiza sukari nje ya nchi na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo  hilo.
Picha ya Pamoja mara baada ya mazungumzo mafupi.

Na Grace Semfuko-maelezo 

Serikali kupitia Shirika la Hifadhi ya Jamii, NSSF na Jeshi la Magereza Tanzania, wapo katika hatua za mwisho za uanzishwaji wa mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Morogoro Vijijini, eneo ambalo linamilikiwa na Jeshi la Magereza 

NSSF kupitia kampuni yao tanzu ya Mkulazi imeamua kuliendeleza shamba hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha sukari, lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa sukari nchini, pia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni za kuagiza sukari nje ya nchi na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo. 

Akizungumza Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani wakati alipotembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio, alisema mradi huo unalenga kuzalisha tani za sukari zisizopungua laki mbili kwa mwaka. 

Alisema pia katika mradi huo watazalisha umeme kwa kutumia mabaki ya miwa kiasi cha megawatt 20 kwa mwaka, kwa ajili ya matumizi ya kiwanda na kuuza TANESCO, kiasi hicho aliongezea kusema kitatokana na uzalisha wa miwa kwa tani milioni mbili kwa mwaka. 

“Sisi NSSF tunafahamu mahitaji makubwa ya sukari katika nchi yetu, Mradi huu mkubwa utaongeza sukari sokoni, lengo letu kubwa ni kuongeza ajira na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa sukari nchini Tanzania,” alisema Bw. Erio. 

Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Said Salim Bakhresa, alizipongeza taasisi hizo za Serikali kwa hatua hizo na akawataka kuendelea kujifunza na kuonesha milango kuwa wazi wakati wowote. 

“Sisi Makampuni ya Bakhresa tupo wakati wote na tutawapa ushauri wa suala lolote mnalotaka kujifunza kwa kuwa tunajenga Taifa moja kiuchumi, milango ipo wazi” alisema, Bw. Bakhresa. 

Bw. Bakhresa ni mwendeshaji wa shamba la miwa ya kufua sukari la Bagamoyo, lenye Hekta elfu kumi lililopo katika eneo la Makurunge, nje kidogo ya mji mkongwe wa Bagamoyo, ambalo lilianza shughuli zake za kilimo cha miwa kwa majaribio mwaka 2018 na kufanikiwa kuvuna tani 864 za miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari. 

Mwezi Oktoba 6, mwaka 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, mara baada ya kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha Bakhresa,aliipatia kampuni hiyo shamba hilo kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo cha miwa, ili kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo. 

Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 mahitaji ya sukari yalikuwa tani 590,000 na kati ya hizo tani 135,000 zilikuwa ni mahitaji ya viwandani na tani 455,000 mahitaji ya kawaida ya binaadamu, ambapo uzalishaji wa sukari nchini ulikuwa tani 350,846 na kuwepo na upungufu wa tani 259,156; hatua iliyoifanya Serikali kuwezesha sekta binafsi katika kuzalisha bidhaa hiyo, na hivyo kiwanda cha Bakhresa pekee kinatarajia kuzalisha tani laki moja za sukari ifikapo mwaka 2022. 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger