Friday, 29 March 2019

Tangazo La Mafunzo Ya Kilimo Nchini Israel

...
UTANGULIZI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatangaza mafunzo katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini Israel. 

Mafunzo hayo ni ya miezi 11 kuanzia mwezi Septemba, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mafunzo hayo yatahusisha pia vitendo (field attachment) kwenye mashamba makubwa ya mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum.

SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI
      i. Awe ni raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 20-35 pamoja na cheti cha            kuzaliwa na Kitambulisho cha Uraia. 
 ii.Awe amehitimu mafunzo ya Kilimo katika ngazi ya shahada ya Chuo Kikuu,                         Stashahada au Astashahada ya Vyuo vya kilimo vinavyotambulika nchini.
iii.Awe na afya njema. 
iv.Awe na ujuzi wa kuandika na kuongea lugha ya Kiingereza.  
 v. Awe na uwezo wa kufanya kazi na watu wa tamaduni mbalimbali. 
vi.Awe tayari kurejea nchini baada ya mafunzo yake.        
                                                       
UTARATIBU WA KUFANYA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yakiwa yameambatishwa na nakala za nyaraka zifuatazo:

     i. Cheti cha kuzaliwa na uraia. 
   ii. Vyeti vya kitaaluma.
 iii.Hati ya Kusafiria au uthibitisho wa maombi ya pasipoti.
  iv.Cheti cha kuthibitisha afya kutoka hospitali inayotambulika.
    v. Barua ya kuonesha sababu za kushiriki mafunzo hayo  (Motivation letter) kwa lugha           ya Kiingereza.
  vi. Wasifu (Curriculum Vitae).
 vii. Picha mbili ndogo (Passport size).
viii. Majina na anwani za wadhamini watatu wanaoishi nchini akiwemo mwalimu wa                 Chuo ulichohitimu.

Maombi yote yatumwe kupitia anwani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Jengo la LAPF
Ghorofa ya 6,
Barabara ya Makole,
S.L.P   2933,
DODOMA.

Au kwa baruapepe; mafunzo.israel@nje.go.tz

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili, 2019

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger