Vongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi
Florence Mwanri (Kulia) wakiangalia moja ya bomba la kusafirishia gesi. Bomba
moja lina uzito wa tani tano na urefu wa mita 11. Mpaka sasa jumla ya kilomita
350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa.
Mhandisi wa Ujenzi kutoka
Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha mabomba ya kusafirishia gesi Timu ya Ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea
baadhi ya maeneo yanakopita mabomba hayo. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati
ya kilomita 492 zimeshatandazwa.
Mmoja wa wakaguzi kutoka Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Nancy Kitajo akistaajabu bomba za
kusafirishia gesi zinazoelekea kwenye kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo
Madimba, mkoani Mtwara.
Mafundi wakiendelea na
ujenzi wa makazi ya wafanyakazi katika kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo
Madimba, mkoani Mtwara.
Timu ya Ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea maendeleo ya ujenzi wa
kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara.
Mhandisi wa Ujenzi kutoka
Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha
michoro ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango ilipotembelea eneo la ujenzi huo, Madimba, mkoani Mtwara. Wanaotazama
ni wakaguzi hao, kutoka kushoto ni Prof. Longinus Rutasitara, Bibi Salome
Kingdom, Bibi Florence Mwanri na Bw. Jordan Matonya.
Mmoja wa viongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Katikati) akitaka
ufafanuzi juu ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo
Madimba, mkoani Mtwara. Wanaomsikiliza ni Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Bibi Salome Kingdom (Kushoto) na Mhandisi wa Ujenzi
kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia).Picha na Saidi Mkabakuli-Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango
--
Na Saidi Mkabakuli
Maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam
unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuendelea
vyema kasi ya kundaza bomba hilo.
Wakizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wahandisi
wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela na
Mhandisi Omary Kitiku wamesema kuwa kasi
ya sasa ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha Madimba,
mkoani Mtwara inatia moyo na hivyo kuashiria kukamilika kwa mchakato huo kwa
wakati.
“Mpaka
sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 za bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam
zimeshatandazwa hali inayokwenda sambamba na mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda
hiki,” alisema Mhandisi Yagela.
Kwa
mujibu wa Mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiko hadi kufikia mwisho wa Julai
kiwanda kinatakiwa kukamilika, na mpaka sasa, makazi ya wafanyakazi imekamilika.
Akizungumza
wakati wa ukaguzi huo, Mmoja wa viongozi wa Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri alisema kwamba kukamilika kwa bomba hilo kunatoa mwanya wa
kukamilika kwa wakati uzalishaji wa umeme katika vituo vya Kinyerezi, jijini
Dar es Salaam.
“Kukamilika
kwa bomba hili kunatoa fursa ya kwa Mradi wa kuzalisha umeme kiasi cha Megawati
150 na Megawati 240 kwa kutumia gesi asilia vilivyopo Kinyerezi, jijini Dar es
Salaam,” alisema Bibi Mwanri.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16),
Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu
ya nishati ambapo nguvu kubwa imewekwa katika uwekezaji wa miundombinu ya
nishati ambapo utekelezaji wa ujenzi wa bomba la gesi Mtwara hadi Dar es Salaam
unafanywa sambamba na ujenzi wa mitambo miwili ya kuzalisha umeme kwa kutumia
gesi katika eneo la Kinyerezi Dar es Salaam.
Serikali
imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za
ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga
watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano
unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa
ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa
ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.
0 comments:
Post a Comment