Sunday 30 March 2014

MVUA ZALETA MADHARA MAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM

...

MVUA ZALETA MADHARA MAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM

Mvua  zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, zimeleta adha kubwa, huku baadhi ya wakazi wakilazimika kuhama baada ya makazi yao kukumbwa na mafuriko.
Gazeti la Mwananchi lilitembelea sehemu mbalimbali jijini jana na kushuhudia mafuriko makubwa, huku baadhi ya nyumba kuta zake zikiwa chini baada ya kuzidiwa na maji.
Kinondoni:wpid-img-20140328-wa0005.jpg
Katika maeneo ya Tanesco Mkoa wa Kinondoni Kaskazini, Msasani Bonde la Mpunga na Mikocheni A Mtaa wa Vyura, hali ilikuwa mbaya zaidi, pamoja na nyumba nyingi hasa za Msasani kuwa nzuri na za ghorofa, lakini zilikuwa zimejaa maji eneo la chini kiasi cha kutoingilika.
Msasani:
Eneo la Msasani ndilo lililoathirika kwa kiasi kikubwa na mafuriko, kwani barabara nyingi hazikupitika kirahisi kutokana na kujaa maji na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.
Maeneo ya Hospitali ya TMJ, Ofisi za Tanesco na Jengo la Biashara la Shoperz Plaza, hali ilikuwa mbaya kutokana na maeneo hayo kujaa maji kwa kiasi kikubwa.
Katika Mtaa wa Vyura Msasani, ambako kuna kliniki maalumu inayotoa matibabu ya figo, maji yalikuwa yamejaa kiasi cha kuwekwa mashine za kunyonya kuyatoa nje.
Tabata:
Katika eneo la Tabata hali ilikuwa mbaya zaidi kwani kuna baadhi ya maeneo magari hayakuweza kupita kabisa kutokana na barabara nyingi kujaa maji.
Daladala zinazofanya safari zake kati ya Tabata Segerea-Mnazi Mmoja, zililazimika kuishia Buguruni kutokana na barabara ya Uhuru kujaa maji na kushindwa kupitika.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger