Abainisha miradi mikubwa ya maendeleo kupitia kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba yake mzazi
Na Lydia Lugakila - Bukoba
Mbunge Rweikiza ametoa ufafanuzi huo wakati akiongea wananchi mbalimbali pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kagera waliofika katika viwanja vya Rweikiza vya shule ya Rweikiza iliyopo Kyetema Wilaya ya Bukoba kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba yake mzazi aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.
Rweikiza amebainisha kuwa,Dkt. Samia Suluhu Hassan amelipendelea Sana Jimbo lake kwani ametoa Mabilioni ya fedha kwa ajili ya maendeleo jimboni humo.
Akieleza miradi hiyo Mbunge huyo amesema kuwa pamoja na Daraja la Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bilioni 9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja hilo kuchoka kwasababu limejengwa muda mrefu.
Amesema Daraja hilo ambalo lipo Barabara kuu inayounganisha kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba,Misenyi na Karagwe Wananchi hulitumia katika kusafirisha mazao na bidhaa nyingine.
Akitaja Daraja lingine amesema ni la Chanyabasa ambapo wananchi hutumia kivuko kuvuka toka kata zaidi ya nane kuja hospitali ya Wilaya ya Bukoba Vijijini na wengime wanaovuka kwenda Bukoba mjini kwa shughuli za kujiingizia kipato jambo linalosababusha watumie muda mrefu wakisubiri kivuko kwasababu kinavusha watu wachache na mizigo kidogo.
Aidha amesema ujenzi huo unaotarajiwa kuanza muda wowote kuanzia hivi sasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12 kutokana na maagizo ya Serikali awamu ya sita.
Ametaja daraja jingine ambalo limeingizwa kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa na fedha yake italetwa wakati wowote kuwa ni Kyetema, linaunganisha
Barabara kuu kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine kuingia Bukoba na nchi jirani ya Uganda.
"Nitumie fursa hii kwa niaba ya Wananchi wa jimbo la Bukoba vijijini nimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake mkubwa kwetu ametoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo yetu"alisema Dokta Rweikiza.
Ameongeza kuwa kuna mradi mkubwa wa maji Kemondo ambao umekamilika na wananchi wanatarajia kupata maji mwezi mmoja ujao.
Naye askofu wa Dayosisi ya kaskazini magharibi (KKKT) Abedinego Keshomshahara amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inafanya maendeleo makubwa kwa Wananchi pia mbunge Rweikiza amekuwa kiungo kizuri kati ya wananchi,Serikali na viongozi wa dini zote.
Kwa upande wa katibu mkuu mstaafu wa chama cha Mapinduzi (CCM),katibu mkuu kiongozi mstaafu,Balozi na mbunge Dkt .Bashir amesema Mbunge huyo ameonyesha mfano mzuri kwa Wananchi wake na Taifa kwa ujumla.
"Maombi ya miradi hiyo ililetwa kwenye chama wakati wa Serikali ya awamu ya tano na mbunge Rweikiza ambapo tuliingiza kwenye Ilani ila kutokana na maono mema ya Rais Dokta Samia ameamua kutoa fedha nyingi ili ikajengwe na kunufaisha Wananchi" alisema Dokta Bashir.
0 comments:
Post a Comment