Tuesday, 24 December 2024

TRA TANGA YAJIVUNIA KUKUSANYA BILIONI 153.6 JULAI - NOVEMBA 2024

...
Na Hadija Bagasha - Tanga

Mamlaka ya ukusanyaji wa Mapato Tanzania TRA Mkoa Tanga imejivunia kukusanya kiasi cha bilioni 153.6 mwaka huu kwa mwezi Julai  hadi mwezi Novemba tofauti na kiwango cha bilioni 78 walichokusanya mwaka jana ndani ya kipindi hicho.


Makusanyo ya kiasi cha shilingi bilioni 153, ni kati ya mambo ambayo Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato TRA Mkoa wa Tanga inajivunia ikiwa na wateja wao mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ziara yao kutembelea wafanyabiashara mbalimbali Jijini Tanga Meneja wa TRA Mkoa Tanga Thomas Masese amesema mwaka 2024 umeanza kwa mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ambapo kuanzia mwezi julai hadi Novemba wamevuka matarajio ya ukusanyaji ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

 “Kwa mikezi mitano hii ya mwanzo kuanzia mwezi julai 2024 mpaka mwezi Novemba tulikuwa na lengo la kukusanya bilioni 131.6 lakini tumekusanya bilioni 153.6 sawa na ufanisi wa asilimia 117,

“Tukitaka kujilinganisha na mwaka jana katika kipindi kama hiki tulikuwa na lengo la kukusanya bilioni 88 tukakusanya bilioni 78 sawa na ufanisi wa asilimia 85 hivyo toka mwaka jana tulipokusanya bilioni 78, mwaka huu tumekusanya bilioni 153 ni ongezeko la takribani asilimia 196.”alisisitiza Meneja Masese.

Wateja waliotembelewa na Mamlaka hiyo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano ,na kuongeza kasi ya ulipaji wa kodi kwa maendeo ya nchi yao huku wakilaani baadhi ya wafanyabiashara wanaokwepa kupila kodi.

“Tunawashukuru TRA kwa kututembelea na kutuona ni walipaji wazuri wa kodi lakini sio tu walipaji wazuri wa kodi lakini tumekuwa mabalozi wazuri mwanzo ilikuwa tukiona TRA tunakimbia lakini sasa wamekuwa ni marafiki zetu nah ii ni kutokana na mahusiano mazuri waliyo nayo kwetu chini ya Meneja Masese aliyepo sasa,”alisisitiza mmoja wa wafanyabiashara hao.

Mamlaka hiyo imeitaka jamii kujenga utamaduni wa kudai risiti mara wanapofanya biashara,ikiamini kama jamii itaimarisha utamaduni wa aina hiyo ,ongezeko la makusanyo mwaka huu yanaweza kuongezeka mara dufu hapo mwakani .

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger