Friday, 18 October 2024

MPASUKO NDANI YA CHADEMA, IKUNGI., MBINU ZA UPINZANI ZAFICHUKA

...

 

 SINGIDA-Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameanza kutibuana wenyewe wilayani Ikungi Mkoa wa Singida huku chanzo kikuu kikitajwa kuwa ni siasa za uadui na chuki zinazoenezwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA- Bara, Tundu Lissu.


Kwa nyakati tofauti mwandishi wa habari hizi ameshuhudia mmoja wa wanachama hicho wilayani hapa akizua taharuki ikiashiria wazi kuwa, tayari siasa hizo za chuki zinazoanzia ngazi ya taifa, sasa zimefika mpaka kwa wanachama wa ngazi za chini.

"Lissu amechochea mgawanyiko kila kona anapopita, na kuacha uhasama mkubwa kutokana na ugomvi wake na Mbowe.

"Lissu, ambaye siasa zake zinalenga kulipiza kisasi na kueneza chuki bila kujali maslahi ya Watanzania, amechagua kutumia mgawanyiko kujinufaisha kisiasa,"amedai mmoja wa wanachama wa chama hicho wilayani Ikungi.

"Hapa Ikungi, ameacha machafuko, akiwaacha wana CHADEMA katika hali ya kuchanganyikiwa baada ya kuwasha moto wa fitina. Hii ni kawaida kwa upinzani kueneza chuki na kugawa jamii bila kutoa suluhisho lolote,"ameongeza mwanachama mwingine huku akionesha kukerwa na tabia hiyo.

Wakati Lissu na wenzake wanadaiwa kuzidi kueneza chuki, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan anaendelea kujenga amani na kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

Miongoni mwa wanachama wa chama hicho na mkazi wa Ikungi anasema kuwa, "Uongozi wake (Rais Dkt.Samia) unalenga kutatua migogoro na kujenga mazungumzo ya kidemokrasia, tofauti kabisa na uharibifu unaosababishwa na siasa za Lissu.

"Mbinu hizi za upinzani kuchochea mgawanyiko ni ishara ya wazi kuwa hawako tayari kuongoza jamii pana ya Watanzania. Lengo lao ni kudhoofisha maendeleo ambayo Tanzania imefikia, na Ikungi ni mfano hai wa jinsi siasa zao za chuki na fitina zinavyoweza kuharibu jamii.

"Ni wazi kabisa kwamba ajenda ya upinzani sio kujenga bali ni kubomoa. Ni lazima tuungane na viongozi kama Rais Samia ambaye anafanya kazi usiku na mchana kuwaunganisha na kuwawezesha Watanzania wote,"ameongeza mwanachama hicho.

Hata hivyo, jitihada za kutaka kupata ufafanuzi kuhusu hali hii ya mtifuano kutoka kwa uongozi wa CHADEMA ngazi ya wilaya na Kitaifa inaendelea. Tazama video fupi hapa chini;
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger