Monday, 21 October 2024

MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA MKOMBOZI KWA MKULIMA

...

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Morogoro wakiangalia miche iliyopo katika kitalu cha kuotesha miche ya Kakao, Karafuu na Chikichi kilichopo katika kijiji cha Kichangani, Kata ya Mhonda, Tarafa ya Tuliani wilayani Mvomero.

........

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imetoa rai kwa wananchi kuutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kutunza na kuuza mazao yao kwa bei halisi ili kupata manufaa na kujenga uchumi kwa ujumla

Aidha, ametoa wito kwa Wananchi hao na kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Viongozi wa Wilaya au Mkoa husika mara wanapoona watu wachache wenye lengo nia ovu yala kuharibu na kudhoofisha Mfumo huo ili kuuimarisha na kuuwezesha kufanya kazi kikamilifu.ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Hayo yamesemwa Oktoba 20, 2024 na Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika ( Mb) wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuona maendeleo katika zao la Kakao na jinsi Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unavyowanufaisha wakulima Mkoani Morogoro

Aidha amefafanua kuwa nia ya Serikali na Kamati hiyo ni kuhakikisha kuwa Mkulima anapata bei halisi na faida kutokana na Mazao yao kama vile zao la Kakao ambalo lililoongezeka bei kutoka Tsh 4,200 mwaka 2021 hadi Tsh 29,595 mwaka 2024

Vilevile, Mwenyekiti huyo imeielekeza Bodi ya Stakabadhi za Ghala (WRRB) kueneza Mfumo huo katika mikoa yote Nchini pamoja na kuongeza aina idadi ya nyingi za mazao yatakayohifadhiwamazao yanatotumia mfumo huo katika maghala kama vile Karafuu na mengineyo ili kuendelea kuwanufaisha Wakulima.

"Nawapongeza WRRB kwa kufanya kazi vizuri na nawataka muendelee kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuwawezesha Wakulima kupata thamani ya Mazao yao. Bodi hii ndio tegemeo katika kumnyanyua Mkulima"

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe akijibu hoja mbalimbali za Wananchi wa Mvomero amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuwakomboa Wakulima kwa kuhakikisha kuwa wanaongeza tija kwenye uzalishaji kwenye eneo dogo, kuongeza thamani na kuwatafutia masoko ya mazao hayo.

Aidha, alitoa wito kwa Wakulima hao kuendelee kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kitumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa manufaa yao huku akiwaasa wasidanganyike kwa Madali wanaonunua mazao kwa bei ya chini bali wawe wavumilivu kwa muda wa siku tatu hadi tano wakisubiri fedha zao baada ya kuuza mazao kupitia Mfumo huo

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amewashauri wakulima kuutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kuwa Mkoa wake unalima mazao mengi kujipanga kuongeza uzalishaji wa mazao mengi ya kibiashara hususani zao la Karafuu ambapo umepanga kugawa kila kaya kuwa na miche 40 ya karafuu ikiwa ni mpango wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo Mkoani humo

Naye Naye Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB Bw. Asangye Bangu amesema Bodi hiyo imepokea maelekezo wajumbe na ameahidi kuwa Bodi hiyo itaendelea kuusimamia Mfumo huo ili kuhakikisha kuwa unawanufaisha wakulima wa mazao yanayopita katika mfumo.

Nao Wananchi wa Mvomero kata ya Turiani wakiongea na Kamati hiyo wamekiri kuwa Mfumo huo ni mzuri na wamefanikiwa kuuza Kakao kwa bei ya tsh 29,000 na 17,000 kwa kilo mwaka 2024 wakati kabla ya kutumia Mfumo huo waliuza Kakao hiyo kwa Tsh 2500 na wameiomba Serikali kuwachukulia hatua wale wote wanaodhoofisha Mfumo huo ili uendelee kuwawezesha kunufaika na bei za ushindani zilizoko sokoni.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Morogoro wakiangalia miche iliyopo katika kitalu cha kuotesha miche ya Kakao, Karafuu na Chikichi kilichopo katika kijiji cha Kichangani, Kata ya Mhonda, Tarafa ya Tuliani wilayani Mvomero.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akisalimiana na akiongea na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo walipowasili Ofisini kwake kwa ajili ya ziara Mkoani humo kwa lengo la kuona maendeleo katika zao la Kakao na jinsi Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unavyowanufaisha wakulima Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe akijibu hoja mbalimbali za Wananchi wa Mvomero wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuona maendeleo katika zao la Kakao na jinsi Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unavyowanufaisha wakulima Mkoani humo.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger