Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Uswisi Bi.Patricia Danzi ,akizungumza na wanufaika wa mpango wa kusaidia kaya masikini (TASAF) katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino wakati wa ziara ya kujionea Maendeleo ya mpango huo kwa wananchi wa kijiji hicho.
Balozi wa Uswisi Nchini Tanzani Bw.Didier Chassot,akiwaeleza wanufaika wa mpango wa kusaidia kaya masikini (TASAF) katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jinsi Serikali ya Uswisi inavyoendelea kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali wakati wa ziara ya kujionea Maendeleo ya mpango huo kwa wananchi wa kijiji hicho.
Mkurugenzi wa wilaya ya Chamwino Dk Semistatus Mashimba,akitoa taarifa ya wanufaika katika miradi ya TASAF katika Halmashauri yake namna wakazi walivyonufaika katika kijiji cha wilunze.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF, Ladislaus Mwamanga,akizungumza na wanufaika wa mpango huo huku akiwataka wananchi kuendelea na kuwekeza katika miradi yao ya kimaendeleo kupitia Miradi ya TASAF mara baada ya kutembelea wanufaika katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino kujionea Maendeleo ya mpango huo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Wilunze Bw.Amos George Chindole,akitoa neno la shukrani kwa Viongozi na wadau wa TASAF kwa kuweza kutembelea na kujionea maendeleo ya Mpango huo katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Wakazi wa Kijiji cha Wilunze wakiwa katika mkutano wa hadhara wakati wa viongozi na wadau wa Mfuko wa Mendeleo ya Jamii TASAF wakizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya Mpango huo katika kijiji hicho.
Muonekano wa ujenzi wa barabara za ndani ya kijiji zilizoanza kujengwa na wanaufaika kwa kutumia zana za mikono
Viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Pamoja na wadau wakikagua mradi wa Barabara uliojengwa na Wanufaika wa TASAF ,inayounganisha Kijiji cha jirani .
Mnufaika wa Mfuko wa Mendeleo ya Jamii TASAF, Mkazi wa kijiji cha Milunze wilayani Chamwino Mkoani Dodoma Bi.Moreni Erenesti,akielezea jinsi alivyoweza kunufaika na mfuko huo.
Mnufaika wa Mfuko wa Mendeleo ya Jamii TASAF,Luzy Agustino,akizungumzia jinsi alivyonufaika na mfuko huo kwa kuwa na makazi yake na malengo yake ya baadae nikujenga nyumba kubwa na Kuendela kusomesha waototo wake ambaye pia anajishughulisha na ujasiliamali (wa kwanza kushoto) ni Balozi wa Uswisi Nchini Tanzani Bw.Didier Chassot (wa pili kutoka kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Uswisi, Patricia Danzi.
Picha ya Pamoja ya wadau na viongozi wa Mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAF baada ya kutembea na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TASAF katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
........................................................
Na.Alex Sonna,Chamwino
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Uswisi, Patricia Danzi amewataka wanufaika wa Mpango wa kusaidia kaya masikini (TASAF) kuwa na mtazamo wa kujikwamua na umaskini.
Danzi ametoa kauli hiyo wakati walipowatembelea wanufaika wa Mfumo wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi huyo amesema kupitia ubalozi wao nchini Tanzania utaendelea kusaidia kuwezesha mambo ambayo yatakuwa kichocheo cha kimaendeleo .
''Serikali ya Uswisi itaendelea kuimraisha ushirikiano na uhusiano wa muda mrefu wa zaidi ya miaka 40 na Tanzani katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo Sekta ya Afya,Elimu pamoja na kusaidia juhudi za Serikali katika mapambano ya kuondokana na umaskini na kuinua kipato cha wananchi''amesema Danzi
Pia ameeleza kuwa Uswisi itaendelea na jitihada zake za kutoa misaada mbalimbali kwa Tanzania ili kunusuru Kaya Maskini.
Danzi amesema kuwa amefurahi kuwasikia wanufaika wakisema kwa uwazi sana, mara nyingi ni vigumu kuongea kuhusu maisha yao, lakini mkiwa na jitihada katika kufanya Kazi mtajitoa kwenye hali ya umaskini.
“Naomba mfanye kazi kwa bidii na maarifa hasa wenye nguzu za kufanya kazi na mjitahidi kujiwekea akiba kwa kidogo mnachopata,”amesema Danzi.
Kwa upande wake Balozi wa Uswisi Nchini Tanzani Bw.Didier Chassot,amesema kuwa Uswisi na Tanzania wamekuwa na mahusiano mazuri na sasa wanasherekea miaka 40 ya ushirikiano .
''Nawaomba walengwa mtumie vizuri fedha mnazopata ili ziweze kuwasaidia nyie pamoja na familia zenu hivyo Kupitia TASAF tutaendelea kushirikiana na Tanzania''amesema Chassot
Awali ,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF, Ladislaus Mwamanga,amesema katika awamu ya kwanza ya mpango wa kunusuru Kaya maskini zaidi ya laki mbili zimefanikiwa kubadilisha hali ya maisha yao hivyo kuondokana na Umaskini.
Hata hivyo Mwamanga ameipngeza wilaya ya Chamwino kwa kutekeleza vyema mpango huo ikiwamo utoaji wa ajira za muda mfupi ambapo yamechangia mabadiliko makubwa kwa wanufaika.
“Kutokana na matokeo mazuri mliyoonesha ndio maana mmepata ugeni huu kutoka Uswisi, niwaambie wametoa Uswisi ni wadau wa maendeleo ambao wametoa msaada mkubwa na wametupatia Sh.Bilioni 41,”amesema.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ana shauku ya kuona wananchi wanaondokana na umaskini.
Naye, Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino, Dk.Semistatus Mashimba amesema kijiji cha Wilunze ni mojawapo ya wanufaika katika miradi ya Tasaf ambacho kinawalengwa 193 na tayari Sh.Milioni 45.1 zimetolewa kwa walengwa kwa mujibu wa mwongozo.
Mmoja wa wanufaika hao, Ruth Kalulu amesema mpango huo umewasaidia kwa kiasi kikubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha ufugaji kwa kuwa mumewe alimkimbia na kumuacha na watoto wanne.
Amesema kwasasa amefanikiwa kujenga nyumba ndogo ya kuishi na familia yake huku ufugaji ukimuingizia kipato kinachosaidia kulipa ada na michango ya watoto shuleni.
0 comments:
Post a Comment