Diwani wa Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo.
Diwani wa Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo
Diwani wa Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo
Diwani wa Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akiwa kwenye mkutano wa hadhara leo
***
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Diwani wa Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Gulam Hafeez Mukadam amepongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata hiyo.
Mukadam amebainisha hayo leo Jumapili Novemba 28,2021 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa wa Buzuka aliouitisha kwa ajili ya kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumchagua kwa kura nyingi uchaguzi uliopita huku akitoa taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mitaa mbalimbali ya kata hiyo.
Amesema wakati wa siasa umekwisha hivyo nivyema wananchi wakajikita kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo huku akiwaomba wakazi wa kata hiyo kuendelea kumuombea na kumpongeza Rais Samia kwa kazi anazofanya badala ya kubeza kazi zake ,waondoe wasiwasi na waendelee kumuamini kwa kazi zake.
“Siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka jana, mlinipigia kura nyingi za ushindi, na kunifanya niwe diwani wenu kwa awamu nyingine tena, ambapo naahidi kuendelea kuwapigania kwa kueleza changamoto zinazoikabili kata ya Mjini na nyinyi mnaona namna barabara zinavy jengwa kwa kiwango cha lami ,ujenzi wa mitaro ,ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari hivyo ni vyema muendelee kuniamini na kumuunga mkono Rais Samia ili aendelee kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali katika kata yetu”, amesema Mukadam.
“Mnachopaswa kufanya kwa sasa ni kumpongeza Rais Samia pamoja na kukemea vikali baadhi ya watu wanaobeza kazi zake ili aendeleze yale mazuri anayo endelea kuyafanya kwa maslahi ya taifa na hasa akina mama msimuangushe Rais Samia ”,ameongeza.
Pia amesema ataendelea kuwaletea maendeleo wananchi kama alivyofanya kwenye awamu iliyopita, na kuibadilisha Shinyanga kuwa Jiji, ambapo Kata hiyo ya Mjini ndiyo kitovu cha mkoa wa Shinyanga.
Hata hivyo amewasisitiza wananchi kujitokeza kupata chanjo ya Uviko 19 kwani ni salama na kuepukana na uvumi wa watu akieleza kuwa hata yeye tangu amechanja yuko vizuri na anaendelea kuchapa kazi.
0 comments:
Post a Comment