Tuesday, 1 June 2021

SMART AFRICA GROUP – KAMPUNI INAYOCHOCHEA MAPINDUZI YA KIDIGITALI, MEDIA NA UBUNIFU

...
Mkurugenzi Wa SAG Bw. Edwin Bruno (mwenye Suti) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara
Smartcodes imezindua kampuni yake mama, Smart Africa Group (SAG) ambayo itakuwa inasimamia idara zake 5 ambazo kwa sasa zimesajiliwa kama kampuni huru na zinakuwa kampuni tanzu.

 Kwa miaka mingi, Smart Codes imekua kutoka kuwa kampuni inayojihusisha zaidi na masuala ya kiteknolojia mpaka ile inayotoa huduma mbalimbali kwenye masoko, teknolojia na ubunifu.

 Sababu kubwa ya kufanya hivi ni kuwa na mhimili madhubuti utakaowezesha mgawanyo wa huduma kulingana na kampuni hizi tanzu 5.

Smart Codes ilianzishwa mwaka 2010 na Ndg. Edwin Bruno. Kampuni ilisajiliwa mwaka 2014 kama kampuni yenye kikomo na kila siku inazidi kukua. Katika muda wote huu, lengo kubwa la kampuni limekuwa ni kuleta mabadiliko ya kidigitali kwa wateja na washirika wetu.

 Hiki hakitabadilika kwa sababu kampuni ina matarajio ya kufanya makubwa zaidi katika mwongozo huu.

“Kuanzishwa kwa SAG kunawezesha kampuni kusimamia ukuaji na kuongeza Imani kwa wateja wetu. Kazi kubwa ya SAG ni kushauri, kuongoza na kuweka dira. Itasimamia utendaji na kuwa maono ya pamoja miongoni mwa kampuni tanzu ili kusaidia kulinda matarajio ya wateja, na pia kuhakikisha kwamba kila kampuni tanzu inaendelea kukua katika kiwango kilichowekwa na Smart Codes hapo kabla. Kwa kuunda SAG, tunawahakikishia washirika wetu kwamba tuna timu bora, mbinu sahihi na taratibu zenye umakini” alisema Ndg. Edwin Bruno, CEO na CVO wa SAG.

Kampuni hizi tanzu 5 zinajumuisha; Smart Codes ambayo inatoa huduma za matagazo na masoko zilizo kamilifu zinazojumuisha upangaji mbinu,huduma za kidigitali, ubunifu, media,shughuli/hafla, hamasa za hadhara na uhusiano kwa umma; Smart lab itaendelea kuwa maabara ya uvumbuzi na kuchochea ubunifu ikihusiana na programu, ujuzi, vipaji na maabara za kuchochea ubunifu; Smart Foundry inahusiana na uundaji wa bidhaa kuanzia utengenezaji wa mbinu, ubunifu, maendeleo na usimamizi; Smart Nology inahusika zaidi na teknolijia katika huduma zetu wenyewe kwa kutoa nyenzo za kutengenezea tovuti, njia za malipo, aplikesheni za simu mpaka kwenye uundaji wa aplikesheni za bahati nasibu; na Smart Studio inatoa huduma za utengenezaji picha na sauti na pia picha za uhuhishaji (animation).


“Lengo kubwa la SAG ni kutengeneza jukwaa litakalowezesha kushirikiana na kampuni za kiafrika katika kuacha alama kupitia teknolojia, media na ubunifu. Haya yote yatawezeshwa na kampuni zetu tanzu 5 zitakazofanya kazi kubwa ya kuhakikisha washirika wetu wanakabiliana kwa usahihi na changamoto zao. Tunaungana na kampuni na chapa za kiafrika zenye lengo la kuleta mapinduzi ya kidigitali. Kama methali ya kiafrika inayosema, “kama unataka kwenda haraka nenda mwenye, kama unataka kwenda mbali nenda na wenzako” alimalizia Ndg. Edwin Bruno, CEO na CVO wa SAG.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger