Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Godfrey Chibulunje,akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa msaada wa mashuka 431 katika vituo vinne vya afya vilivyopo Jiji la Dodoma hafla iliyofanyika leo June 23,2021 jijini Dodoma na kuhudhuruliwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dk. Andrew Method.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Godfrey Chibulunje,(kulia) akimkabidhi sehemu ya mashuka Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dk. Andrew Method baada ya EWURA kutoa msaada wa mashuka 431 katika vituo vinne vya afya vilivyopo Jiji la Dodoma hafla iliyofanyika leo June 23,2021 jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma,Dk. Andrew Method ,akitoa neno la shukrani kwa EWURA baada ya kupokea msaada wa mashuka 431 katika vituo vinne vya afya vilivyopo Jiji la Dodoma iliyotolewa na EWURA hafla iliyofanyika leo June 23,2021 jijini Dodoma.
Muonekano wa maboksi yakiwa na mashuka yalitolewa na EWURA
.................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), imetoa msaada wa mashuka 431 kwa vituo vinne vya afya vilivyopo Jiji la Dodoma yenye thamani ya Sh.Milioni tano,ili kusaidia uboreshaji wa huduma za afya katika jiji hilo ambalo linakabiliwa na ongezeko la idadi ya watu.
Akitoa msaada huo leo June 23,2021 jijini Dodoma ,Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Godfrey Chibulunje,amesema kuwa wametoa msaada huo ili kuongeza kasi ya utoaji huduma za afya kwa wananchi kupitia vituo vya afya vinne ambavyo ni Makole, Mkonze, Hombolo na Kikombo.
Mhandisi Chibulunje amesema kuwa msaada huo wameutoa ikiwa ni mchango wa EWURA kwa jamii hususan katika kipindi hiki cha kuhitimisha wiki ya utumishi wa umma nchini.
Amesema kuwa msaada huo utasambazwa katika vituo vya afya vilivyolengwa kwa kuzingatia mahitaji halisi katika kila kituo.
“Tumetoa msaada wa mashuka 431 kwa Jiji la Dodoma na yataenda kwa vituo vinne cha Makole, Hombolo, Mkonze na Kikombo, tumechangua mwaka huu eneo la afya ili kusaidia mwaka mwingine tutachagua eneo jingine,”amesema Mhandisi Chibulunje
Mhandisi Chibulunje amesema katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma, mamlaka hiyo imetoa mafunzo kwa watumishi wake na kutembelea watoa huduma mbalimbali wanaowasimamia kubaini changamoto wanazokabiliana nazo ili waweze kuzitatua
''Lengo letu ni kuhakikisha mlaji anapata huduma bora kwa viwango vinavyosimamiwa na mamlaka yetu''ameeleza
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dk. Andrew Method,amesema kuwa Jiji hilo linashukuru kwa msaada huo kwa kurejesha katika jamii kwenye sekta ya afya.
Dk.Method amesema kuwa kwa wastani katika Kituo cha Afya Makole, wajawazito 120 wanajifungua kila wiki, hivyo kwa mwezi idadi ya wajawazito wanaojifungua katika kituo hicho inafikia 400 hadi 600.
''Tutahakikisha msaada huo unatumika katika maeneo yaliyokusudiwa huku akiishukuru EWURA kwa kuendelea kusaidia sekta ya afya kwa jiji hilo ambapo tayari ilikwishatoa msaada wa vifaa vya kutunza watoto njiti.''amesema Dk.Method
0 comments:
Post a Comment