Tuesday, 2 June 2020

WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WAPEWA VIFAA KUJIKINGA NA CORONA

...

Rais wa umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania Deogeatius Nsokolo akimkabidhi mwanachama wa chama cha waandishi wa habari matukiodaima mkoa wa Kigoma Editha Karlo vifaa vya kujikinga na virus vya corona anayeshuhudia ni katibu wa kigoma press Club Mwajabu Hoza : Picha na Kigoma Press Club 
Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari (UTPC) Deogratius Nsokolo kushoto akikagua vifaa vya kujikinga na virusi vya corona vilivyotolewa na wadau mbalimbali pamoja na UTPC kwa ajili ya wanachama wake.
Na Editha Karlo - Kigoma

CHAMA cha waandishi wa habari wa Mkoa Kigoma(KGPC)imegawa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa wanachama wake ili kuwasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Vifaa hivyo vimetolewa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)kupitia mpango wa utekelezaji wa mpango mkakati wa kuzisaidia club za waandishi wa habari unaodhaminiwa na shirika la maendeleo la Sweden(SIDA).

Mratibu wa Klabu hiyo Diana Rubanguka alisema kuwa kila mwanachama atapata barakoa,glavu,chupa ya dawa ya kutakasa mikono(sanitaizer)ambavyo vitawasaidia kujilinda na kujikinga na ugonjwa huo.

Diana alisema vifaa hivyo vimetolewa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kupitia mpango wa utekelezaji wa mpango mkakati wa kuzisaidia club za waandishi wa habari unaodhaminiwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA).

Rais wa UTPC, Deogratias Nsokolo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma alisema kuwa kutokana na hali ya mlipuko uliopo sasa wa ugonjwa virusi vya corona walikubaliana na SIDA kutumia baadhi ya fedha kununua vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo na kutoa mafunzo kwa wanachama juu ya ugonjwa huo.

"Baadhi ya mambo yaliyokuwa yafanyike mwaka huu yamehairishwa na fedha zilizokuwa zimetengwa zimeelekezwa upatikanaji wa vifaa hivo kwaajili ya club zote za Tanzania Bara na visiwani",alisema Nsokolo.

Alisema kazi za waandishi wa habari zinahitaji kukutana na watu mbalimbali hivyo ni muhimu kuwa na vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo.
Nsokolo aliwataka wanahabari wote nchini kuendelea kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kuzingatia na kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na serikali ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa hivyo kwa ufasaha.

Baadhi ya wanachama wa KGPC wakizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo wamesema kuwa wameupongeza uongozi wa club yao na UTPC kwa kuzingatia na kuona usalama wa wanachama wao wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger